SHAMSHA FORD ALIAMUA KUISHI NA CHIDI MAPENZI KWA SABABU ALIKUWA HANA UHAKIKA NA AFYA YAKE

Baada ya kufahamika kuvunjika kwa ndoa ya Shamsa na Chiddi Mapenzi, Muigizaji, Mwijaku ametoa maneno yake kuhusu ndoa hiyo.

Mwijaku amesema hivi, Shamsa Ford aliamua kuishi na Chiddi akiwa hana uhakika na afya yake hivyo amechezea bahati kwasababa mwanamke huyo alikuwa amemaliza ujana.

"Chiddi mapenzi tangu ameanza kuwa na Shamsa Ford alikuwa amenawiri alikuwa hana upaukaji, Shamsa alikuwa anajua kumhudumia alikuwa anahakikisha anakunywa dawa zake vizuri na anakula kwa wakati, lakini watu wengine wanatakiwa wajue kupata maradhi ya Ukimwi ni kuamua," Mwijaku ameiambia EATV.

"Chiddi Mapenzi amechezea bahati, Shamsa Ford alikuwa ameshamaliza ujana , alikuwa amekaa kwaajili ya maisha ameacha Mke mwema anaanza kuwakimbilia Ma Slay Queens kitamtokea puani. Nakupa miezi mitatu anguko la Chiddi Mapenzi linakuja , wanasema mkataa pema pabaya panamuita na malipo ni hapa hapa duniani kwa Mungu ni mahesabu tu , Shamsa Ford aliamua kuishi na Chiddi akiwa hana uhakika na afya yake."

Post a Comment

0 Comments