SANCHI USIPOMJUA LAZIMA UNYWE PANADOL

Sanchi Usipomjua lazima unywe Panadol

MWANAMITINDO maarufu Bongo ambaye jina lake limekua kutokana na kuvaa nguo zinazomuonesha maungo yake wazi, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amesema kuwa, kama mtu hamjui, lazima kichwa kitamuuma.

Sanchi aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, kuna mtu hamjui kabisa zaidi ya kumuona mitandaoni na picha zake hivyo lazima ajiulize mengi na mwisho aumize kichwa chake.

“Unajua unaponiona tu kwenye mitandao, lazima kwa kweli kichwa kikuume hivyo kuhitaji Panadol kwa sababu tu utachukua muda mwingi kunitafakari bila sababu za msingi hivyo ninawashauri wanaonitafakari na kuniwazia waache watatapika damu bure,” alisema Sanchi.

Post a Comment

0 Comments