LULU: TUJIFUNZE KUJIKUBALI WENYEWE


LULU: TUJIFUNZE KUJIKUBALI

MWIGIZAJI mwenye nyota ya kipekee Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa hakuna kitu kizuri kama mwanamke kujiamini maana hiyo ndiyo silaha yake kubwa. Akizungumza na Amani, Lulu alisema wanawake wengi wanakuwa hawapendi kujikubali, mwingine anaogopa hata kutoka nje bila kujiremba kwa sababu anaamini bila kufanya hivyo haonekani mrembo.

“Mimi naamini kabisa kila mwanamke akijiamini atafanya vitu vingi vikubwa duniani kama siku hizi wanawake au hata mastaa hawawezi kutoka bila kujiremba hiyo ni kukosa tu kujiamini,” alisema Lulu

Post a Comment

0 Comments