SABABU ZA MAUMIVU BAADA YA TENDO

Kuna wanawake wanapofanya mapenzi huhisi maumivu, hakika husumbuliwa sana. Mwanamke anaweza kukosa furaha na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni, ukeni au ndani zaidi na huwa ya aina mbili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo la ndoa kama tulivyofafanua hapo juu na pili ni baada ya kufanya kufanya tendo la ndoa au mapenzi.

Yale maumivu anayopata mwanamke wakati wa tendo la ndoa hutokea pale mwanamke anapoanza kukutana kimwili na mwanaume na mara nyingi hutokana na uke kuwa mkavu sana. Hii inaweza kusababishwa na maandalizi hafifu kabla ya tendo lenyewe na matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko wa hamu ya tendo hilo.

Wataalam hugundua kuwa mara nyingine husababishwa na misuli ya uke kubana ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo lenyewe kutokana na kumbukumbu mbaya za nyuma.

Kwa wale wanawake waliokeketwa huweza kukumbwa na maumivu wakati wa tendo hili kutokana na kuwa na makovu ukeni baada ya vidonda kupona kutokana na athari za kukeketwa. Uwepo wa michubuko na vidonda au maambukizi ukeni, mfano kama fangasi za muda mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono nayo husababisha mwanamke kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri pia huchangia.
SaBaBu Nitataja sababu hizo kwa maelezo mafupi; Kukakamaa kwa misuli ya uke (vaginismus): Hali hii inasababishwa na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha. Matatizo ya shingo ya kizazi; Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi na kusababisha maumivu. Matatizo katika mfuko wa uzazi kama ya Fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Maambukizi ya uke; Aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile maambukizi ya fangasi yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.

Endometriosis; Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za mji wa mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi, hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili. Matatizo ya Ovari. Matatizo haya ni pamoja na uvimbe kwenye mfuko wa mayai yaani Ovarian Cyst.

Wanawake waliokoma kupata hedhi, Menapause, maumbile yao yanasinyaa na kuwa makavu, hivyo kuchochea maumivu wakati wa tendo la ndoa. Magonjwa ya zinaa; Magonjwa ya zinaa kama malengelenge Herpes, masundosundo n.k, yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

TIBA Ili kujua tiba ni lazima uende kuonana na daktari ambaye atakupima na kugundua tatizo lako kisha atakupa dawa stahiki.

Post a Comment

0 Comments