NJIA ZA KUMMILIKI MPENZI WAKO ASIENDE KWA MCHEPUKO

Leo ni siku muhimu ya kujifunza mbinu ambazo huwafanya wanaume kujisikia wako ulimwengu mwingine wakati wa tendo la ndoa.

Kuna umuhimu mkubwa kwa mwanamke kujifunza mambo haya na kuyafanyia kazi ili kumdhibiti mpenzi wako akaachana na michepuko.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa wanaume walio wengi kuwa na nyumba ndogo, hii yote ni katika kutafuta mapenzi motomoto ambayo yatampagawisha.

Wanawake walio wengi leo hii wamejisahau sana kwa wapenzi wenu kiasi cha kwamba wanatoka nje ya mahusiano.

Jambo la kwanza la kuliangalia ni Usafi wa mwili kabla ya kufanya tendo la ndoa lazima mwanamke uhakikishe mwili wako upo safi.

Tunaposema mwili kuwa safi ni kuoga mwili mzima, kusafisha sehemu zako za siri pamoja na maeneo yote ambayo yamejificha wanaume walio wengi na wanaojua mapenzi hupenda kuzichezea sehemu hizo kwa kuwa ndizo ambazo huhifadhi mihemko ya mwanamke.

Baadhi ya wanawake hujisahau kujisafisha vizuri na kutoa jasho lililopo katika miili yao bila kusafisha sehemu nyenginezo ambazo hutumika katika suala nzima la tendo la ndoa.

Kama utakuwa na harufu za baadhi ya maeneo katika mwili wako jua humpunguzia mwanaume hamu ya kufanya mapenzi.

Hakikisha masikio na kitonvu chako vipo safi. Pia hakikisha sehemu ya magoti yako kwa nyuma zipo safi.

Jambo jingineni Usafi wa chumba hakikisha unasafisha chumba au mahali ambapo umepaanda kwa ajili ya kuja kumliwaza mwenzi wako kabla hajafika eneo la tukio.

Unatakiwa kutandika kitanda vizuri kwa shuka zenye rangi ya kuvutia ambazo zinamshawishi mwanaume na sio kutandika shuka zenye rangi za huzuni.

Weka chumba chako manukato mazuri kama ni wakati wa usiku kuna mishumaa ambayo ina manukato ya kimahaba unaweza kuiwasha.

Jambo jingine jifunze kumtega mpenzi wako kwa kumvalia nguo fupi mnapokuwa chumbani hii humfanya mwanaume kupata mihemuko kila anapokuona.

Pia humuandaa kisaikolojia na kuufanya mwili wake kuwa tayari pindi utakapohitajika. Baadhi ya wanawake hupenda kuvaa nguo fupi watokapo na kuwaonyesha watu wengine sehemu zao muhimu lakini hawafanyi hivyo kwa wapenzi.

Muonyesho mumeo kwamba hakubahatisha kukuchangua wewe na unatakiwa kuhakikisha nguo zako za ndani kama chupi na sidiria zipo safi na zenye mvuto.

Jambo jingine jitahidi Usimuudhi mpenzi wako: Hakikisha usimuudhi mpenzi wako kwa jambo lolote ikiwemo kutumia lugha chafu, kumzungumzia na kumsifia mwanaume mwengine, mpambe mpenzi wako kwa majina mazuri (Baby, honey, my sweet, my bae, my cholate, my love, my everything, my heart) kabla ya tendo.

Kuna baadhi ya wanawake huwaita waume zao majina mazuri wakati wanapopewa zawadi tu au wakati wanapofikishwa kileleni hii sio sawa kabisa.

Mwanaume aweze kukufikisha kileleni anahitaji maandalizi upo mwali, muandae kwa kumuita majina mazuri ili ajisikie furaha mwili upate kutulia kwani wengine huwa wameudhiwa huko walipotoka sasa unatakiwa kumtoa alipo na kusahau kabisa.

Post a Comment

0 Comments