Una miaka mingapi?
Utakua umeshituka kidogo hapo! Je huko proud na miaka yako?
Msanii na video vixen nchini Gigy Money siku ya leo anatimiza miaka 22 ya kuzaliwa kwake.
Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ameamua kuifanya kwa tofauti kwa kuonyesha watu hadi cheti chake ili kuthibitisha miaka yake ambayo inakuwaga utata sana anapohitaja na kuzua taharuki.
Miaka mitatu hivi imepita pale wabongo mitandaoni waliposhitushawaga na mshangao baada ya inteview moja hivi Gigy kudai kuwa ana miaka 19 mitandao yote ilijaa kwa watu kubisha na watu kuamua hadi kuitengenezea vituko kauli hiyo.
Kupitia akaunti yake ya instagram Gigy Money ameweka a video aliyojirekodi na kuwananga wale wote wanasomsema ana umri mkubwa wakati yeye ana miaka 22 tu mpaka sasa
Gigy Money aliambatanisha na ujumbe huu kwenye hiyo video
Mkitaka Na Passport ntawapostia Na mama angu ntawapa mumfamyie Interview 🤣
Wadau kadhaa mtandaoni wameonyesha kumuunga mkono staa huyo na madai yake hayo ambayo wengi hawayaamini wakidai kuwa anaficha umri wake halisi;
Hahahahahahahaha dada gigy mm najua ww mdogo sana ni shida tuuu ndo zinakufanya unakua mkubwa na mambo yako ni ya kikubwa kubwa😅😅😅😅
mi Gigy naelewa umemaliza form 4 juzi tu hapa 18 + 4Yrs ni 22 aina kubisha
😂😂😂😂😂😂😂 Dah chambo hilo na evidence 😂😂
Licha ya staa huyo kuonyesha cheti chake kwenye video hiyo wadau wamekataa kabisa ushahidi huo na kudai kuwa vyeti vinatengenezwa na wengine kudaii mbona umbo na sura yake vinaonyesha ana zaidi ya miaka 25, cheki hapa maoni ya wadau hao.
Vyet vinatengenezwa asee me nimezaliwa 1990 nina chet cha utafutaji nimeandika 2001 pumbavu wew
Shida sura yako na matendo yako gigy vinaonekana ni30+
Sasa kama miaka 22 umekuwa hivyo ukifika 50 …??
Mie pia nimezaliwa 1990 ila cheti chngu 1993 mpaka passport kuna kitu kinashindikana siku hizi 😁😁😁
Gigy Money na Baby Wake Mpya.
Mjue zaidi msanii huyu na vituko vyake kupitia moja ya interview alizowahi kufanya, hii hapa ya Milard Ayo;
0 Comments