Kama unajihisi kwamba huna hamu kabisa ya kufanya tendo la ndoa, usihofu, sababu kuna njia nyingi tu za kuhakikisha unakua na hamu ya tendo.
Kuna wakati watu wengi hujikuta wana hamu ya tendo lakini kuna wakati mwingine inapotea kabisa yaani hali inakua inabadilika badilika.
Tafiti zinaonyesha, nusu ya wanawake duniani wanakumbwa na matatizo aidha kutokua na hamu ya tendo au kutofika kileleni katika wakati Fulani kwenye maisha yao.
Wanaume pia hupata tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo au kuwa na hamu katika kiwango kidogo sana.
Wataalamu wa masuala ya ngono, wamezitaja njia mbali mbali za kuongeza hamu ya tendo. Lakini kwanza tuangalie, nini kinasababisha mtu asiwe na hamu ya kufanya mapenzi?
Sababu zinazopeekea kukosa hamu ya Tendo
Vitu vingi vinaweza sababisha tatizo hilo ikiwemo msongo wa mawazo, homoni kuwa chache na hata mazingira kiujumla ambapo hujumuisha matatizo ya kifamilia.
Vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanawake pia vinaweza kuathiri ingawa si wanawake wote wanapata tatizo hilo.
Sababu nyingine ni kama kuwa na uzito uliopitiliza, uvutaji wa sigara, uchovu, matatizo ya kiafya na maradhi na hata matatizo katika mahusiano.
Chantelle Otten, Mtaalamu wa Masuala ya ngono anazungumzia mtu kutamani sana kusisimuliwa kuwa ni tatizo sababu mwisho wa siku linakata stimu. Unaweza kuta mtu anapania asisimuliwe, aandaliwe ili awe tayari kwa tendo. Lakini kufanya hivyo kunaweza kuleta matokeo tofauti kwani unaweza kuta stimu zinakata.
Nini Cha kufanya
Kwanza chunguza ujue nini kinakusababishia kukosa hamu ya tendo la ndoa, ukishagundua tu unaweza kuanza tafuta suluhu au tiba.
Baadhi ya mambo ya kufanya ni kupunguza msongo wa mawazo, kufanya mazoezi, kupunguza uzito, kupata ushauri kama kuna matatizo katika ndoa/ Mahusiano na kubwa ni kuhakikisha mawasiliano kati yako na mwenzi wako yako vizuri.
Chantelle aliwashauri wapenzi kuchukua muda wanapokua faragha, wasiwe na haraka haraka, wafanye mambo taratibu.
Mbali na hilo, ameshauri kufanya tendo kwa kutulia, bila kuwa na wasi wasi au woga wowote, hali hiyo itaruhusu wapenzi kuweka akili zao kwenye tendo na si pengine na hiyo itawasaidia kuwapa hamasa ya kuendele kufanya na kufurahia tendo.
0 Comments