Watu wengi hujikuta wanakosa usingizi wakati wa usiku kwa kua na msongo wa mawazo au hata kutokea tu mtu anasumbuliwa na tatizo la usingizi.
Wengi uhangaika ili wapate usingizi walau hata kidogo ili kesho yake wapate kuamka akili ikiwa imetulia.
Kama unasumbuliwa na tatizo la usingizi basi jua haupo peke yako, na bahati nzuri, kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzi jaribu, na zikakusaaidia kupata usingizi mzuri na haraka kila siku. Soma njia hizo hapa chini:
Hakikisha chumba chako hakina mwanga mkali
Kuhakikisha kuna mwanga mdogo sana au kuzima kabisa lisaa limoja kabla ya kulala kutakusaidia kupata usingizi haraka, tunapozungumzia mwanga mkali tunajumuisha mwanga wa simu au vifaa vyovyote vya umeme, hivyo hakikisha mwanga ni mdogo.
Punguza Kelele
Jitahidi kupunguza kelele chumbani kwako kadri uwezavyo, kwa mfano, kama una saa ya ya kizamani ambyayo utembeajiwake tu ni kelele iondoe na iweke saa isiyo na makelele. Au kama unaishi na mtu, muombe apunguze maongezi, au sauti ya mziki au kipindi cha TV.
Hakikisha chumba hakina joto sana
Joto likizidi alo mtihani, unaweza hangaika na usipate usingizi. Hivyo basi jitahidi kupunguza joto hilo, aidha kama una madirisha makubwa yafungue, kama una feni ama AC iwashe.
Soma kitabu
Kusoma kitabu ukiwa kitandani kunaweza kukusaidia kupata usingizi haraka, kukaa kitandani bila kufanya chochote hali ya kuwa hunanusingizi kunaweza kukuzidishia msongo wa mawazo tuu. Kusoma kitabu kilichochapishwa badala ya simu yaweza kua njia nzuri zaidi.
Jaribu kuhesabu
Unaweza kuhesabu namba, kuanzia namba kubwa halafu unakuja mpaka ndogo kabisa,mfano toka mia moja mpaka moja, fanya hivyo taratibu, waweza jikuta unapata usingizi kabla hujamaliza namba.
Jiekee muda maalum wa kulala.
Wakati mwingine, kubadili muda mara kwa mara kwaweza kuwa ni tatizo, kujiekea muda maalum wa kulala na kuamka kunaweza ufanya mwili wako uzoee ratiba hivyo isiwe shida kulala. Hivyo kama huwa unalala saa 3, hakikisha kila saa tatu unaenda kulala, kadhalika kwenye muda wa kuamka.
Zima vifaa vya umeme lisaa limoja kabla ya kulala
Ukijijua usingiz kwako ni tatizo ni vyema ukazima simu mapema kuliko kujiingiza kwenye mitandao y akijamii na kupotelea huko kuja kustuka ni asubuhi. Kujichanganya kwenye mitandao ya kijamii wakati unatafuta usingizi kunaweza kukuongezea stress. Mbali na hivyo mwanga wa simu pia si mzuri, unaweza kukuondoshea usingizi, na kama utalazimika kutumia simu basi tumia mwanga mdogo sana.
Njia nyinginezo
Mambo mengine ni kama vile kula mapema, kuepuka mazoezi wakati wa usiku, epuka vinywaji vyenye Caffein kama vile kahawa na energy, hakikisha chumba chako kiko vizuri, usiwe kama unalala stoo, kunywa kitu cha moto kama maziwa au chai ya rangi,
Watu wengi sana wamezungumzia kuwa, kuweka kitunguu swaumu chini ya mto kunaweza kukusaidia upate usingizi na kulala vizuri. Unachotakiwa kukifanya ni kuweka punje ya kitunguu swaumu chini ya mto kabla haujalala na ukiamka basi ukitoe, na kesho uweke kingine tena.
Tatizo likizidi, ukiona unajaribu njia zote lakini kila siku usingizi kwako ni tatizo basi muone daktari.
0 Comments