MPENZI WA RAYVANNY ATANGAZA TAREHE RASMI YA HARUS YAO

Mwanamuziki nyota ambaye amevuma kwa kibao cha Mwanza Nyegezi Rayvanny na mpenzi wake wa dhati wanatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni

Habari hii njema ilitangazwa na mpenziwe Rayvanny, Fahvany kwenye ukurasa wake wa Instagram na tayari imepokelewa vema na wafuasi wao.

Fahvany alifichua kuwa yeye na mpenziwe wanapanga kufanya harusi ya kufana Jumapili Julai 7, 2019.

Mama huyo mwenye mtoto mmoja alichapisha picha ya gauni atakayoivalia siku ya harusi yake na kuwasihi wafuasi wake watenge siku hiyo ili waweze kuhudhuria harusi yao.

Fahvany amekuwa akimuonyesha Rayvanny mapenzi tele ila kuliwahi kuwa na tuhuma za mwanamuziki huyo kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao wa kimapenzi.

Rayvanny aliwahi kashifiwa kwa wakati mmoja kwa kuwa na wapenzi wengi wakiwemo wazungu, madai aliyoyakana vikali.

Post a Comment

0 Comments