MKE WA MAREHEMU MENGI (K-LYN) AZUA SIMANZI MPYA


 K-KYNN AIBUA SIMANZI UPYA

DAR ES SALAAM: SIKU chache baada ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi kufariki dunia na kuzikwa, mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lynn’ ameibua simanzi upya baada ya kuandika ujumbe maalum wa kumkumbuka marehemu mumewe. K-Lynn aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mei 28, mwaka huu ambapo ujumbe huo ulilenga kumtakia heri ya sikukuu ya kuzaliwa marehemu Mengi. Ujumbe huo aliouambatanisha na kadi iliyokuwa na mishumaa na maua ulisomeka hivi:

“Today we would have been celebrating you, if I close my eyes I can see how you would have smiled when we sing happy birthday to you. There are no words to describe how much I and the kids miss you, waking up each day without you. Happy birthday my true love, forever in our hearts.”

Tafsiri isiyo ya moja kwa moja: “Leo tunasherehekea siku yako, nikifumba macho yangu ninaona jinsi ulivyokuwa unatabasamu tulipokuwa tunakuimbia wimbo wa bethidei. Hakuna maneno yanayotosha kuelezea jinsi mimi na watoto wetu tunavyokukumbuka, tunaamka kila siku asubuhi bila uwepo wako. Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu wa kweli, milele ndani ya mioyo yetu.”

Kitendo cha kuandika ujumbe huo kiliibua simanzi upya ambapo wachangiaji mbalimbali wa mtandao huo walieleza hisia zao huku wengine wakiweka alama za kulia machozi kuonesha jinsi gani wameguswa na ujumbe huo. “Angekuwa hai na yeye angejibu: “Thank u my wife Jack, I love u crazy,” aliandika Kulthum Matanda huku akimalizia na ‘viemoji’ vya kuonesha ishara ya kulia. “Pole sana J. Ntuyabaliwe maana kuondokewa na mtu uliyemzoea inauma sana cha muhimu ni kumuombea tu apate pumziko la milele amina,” aliandika Leon Swai. Mbali na wawili hao, maoni mengi yaliyoendelea kuwekwa katika ujumbe huo yalikuwa ni ya kumsikitikia K-Lynn na kuonesha jinsi walivyoguswa na kifo cha Mengi.

Post a Comment

0 Comments