MAMBO WANAYOKOSEA WANAUME WAKATI WA KUTONGOZA

1:KUWA NA SUBIRA
Baadhi ya wanaume wanapomtonga mwanamke wanakuwa na papara yaani anakuwa na haraka jambo ambalo husababisha hukataliwa.

Embu jitahidi kuacha papara unapomtaka mwanamke nenda naye taratibu usiwe na haraka ya kupewa majibu ya kukubalika katika mahusiano kwa muda mfupi.

Kuna baadhi ya wanaume ni waajabu anakutongoza leo ndani ya muda mfupi anataka ukampe penzi hii haipo sawa. Ni vizuri ukazuia tamaa zako utasababisha hata huyo mwanamke akuogope na kuhisi huenda una magonjwa.

ISHI UHALISIA
Wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu. Ukiwa unamtonza mwanamke onyesha uhalisia wa maisha yako usitake kujionyesha upo matawi ya juu wakati una shida zako nyingi.

Wapo ambao wanadanganya hadi kazi wanazozifanya ilimradi tu aonekane yupo viwango vya juu jambo ambalo litamletea shida katika hayo mahusiano.

Ni vizuri kuwa mkweli katika mahusiano maana unapokuwa unajifanya viwango vyako ni vya juu utasababisha huyo mwanamke akupige mizinga mikubwa.

Wakati ungeeleza ukweli akakujua angekuchukulia jinsi ulivyo sasa unajikuta unateseka kwa maisha ya kulazimisha.

3:MSOME MWANAMKE YUPO KATIKA HALI GANI
Unapomtongaza mwanamke jambo la kwanza unatakiwa kumsoma yupo katika hali gani wakti mwingine kuna shida inamsumbua wewe ukianza kumsomesha lazima akutose.
4:KUMPONDA DEMU WAKO WA ZAMANI

Epuka kumzungumzia mwanamke wako wa zamani kwa mpenzi mpya. Unapoulizwa mbona upo single usianze kumponda demu wa zamani na kuanza kutoa maneno ya kashfa.

Hali hiyo inaweza kumtisha unayemtongoza na kujikuta unapewa majibu ya kukataliwa.
5.KULALAMIKA
Wanaume wengine utakuta unamtongoza mwanamke huku unalalamika hujawahi kupendwa hapo unaonyesha udhaifu wako.

Jifunze kumtongoza mwanamke bila kuonyesha madhaifu yako kama hujawahi kupendwa na mwanamke utakuwa na matatizo yako binfsi na sio kila unayemtongoza unaanza kumuelezea udhaifu wako.

Ukitulia na kumtongoza mwanamke bila kuyatenda hayo utampata mwanamke ambaye unampenda kweli kutoka moyoni mwako.

Post a Comment

0 Comments