KWANINI MAZOEZI YA VIUNGO NI MUHIMU SANA KWA NGUVU ZA KIUME?

Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym.

Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama.

Jina langu naitwa fadhili paulo. Endelea kusoma ….

Wanaume napenda mfahamu tunapozungumzia nguvu za kiume hatuzungumzii nguvu za uume, bali tunazungumzia nguvu za mwili na siyo nguvu za uume kama uume.

Mwili una vyanzo vikuu vitatu vya nguvu ambavyo ni;

1. Chanzo kikuu cha kwanza cha nguvu cha mwili ni SUKARI. Hapa ni sukari yenyewe kama ilivyo sukari au vyakula kama vya wanga na protini hubadilishwa na kuwa glukozi au sukari ambayo ndiyo nguvu ya mwili

2. Chanzo cha pili cha nguvu ya mwili ni MAFUTA. Na hiki ndiyo chanzo pekee cha nguvu cha mwili chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko chanzo kingine chochote cha nguvu cha mwili. Hivyo ukisema watu wasile mafuta ili wapate nguvu umepotea sababu mafuta yenyewe ni chanzo cha nguvu chenye uwezo wa kukupa nguvu kuliko vyanzo vingine viwili vya nguvu vya mwili

3. Chanzo cha tatu cha nguvu za mwili ni MAJI NA CHUMVI. 

Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, ‘cation pumps’, ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.

Inajionyesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu.

Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo, njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari.

Njia hii ya pili huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluconeogenesis’, yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa. Utengenezaji wa aina hii ya sukari hufanyika katika Ini.

Hivyo ni vigumu mtu kuishi bila mafuta, wanga au sukari

Kwanini mafuta ni mhimu katika kutengeneza nguvu za mwili?

Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati(nguvu), kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati(nguvu). Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa na anakuwa na nguvu nyingi zaidi kuliko kama maji/chumvi au sukari/wanga/protini vikitumika kuzalisha nguvu

Kwahiyo utaona mafuta yana uwezo wa kukuletea nguvu za mwili mara 2 zaidi kuliko vyanzo vingine viwili vya nguvu vya mwili

Sasa shida ipo hapa. Mwili kamwe hauchagui mafuta kama chanzo chake cha nguvu isipokuwa tu umefanya mazoezi ya viungo au umefunga kula chakula masaa kadhaa. 

Bila kufanya MAZOEZI AU KUFUNGA KULA mwili utaendelea kuchagua SUKARI kama chanzo chake cha nguvu na mafuta yataendelea kujirundika mwilini bila kuwa na faida yoyote na hivyo kukuletea kitambi, manyama uzembe na mwisho kukuletea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kwahiyo ukikutana na mtu anakuambia usitumie mafuta ili kuwa na nguvu za kiume anakudanganya. Mafuta ni mhimu kwako kama ilivyo mhimu pia vyakula vya wanga na protini lakini ni lazima uwe bize na mazoezi ya viungo kila siku ili kupata faida hii adimu ya mazoezi ya viungo kwa nguvu za mwili na kiume kwa ujumla.

Mafuta nayo yamegawanyika mara mbili. Kuna mafuta mazuri na mafuta mabaya.

Kwa mfano mafuta yanayotumika kupikia chipsi au maandazi au mafuta mengi tunayotumia kupikia majumbani si mafuta mazuri. Hata nafuta ya alizeti si mafuta mazuri kwa afya ingawa hili wajasiriamali wengi wa mafuta ya alizeti hawataki kulisikia ukilisema kwani wanaona unawaharibia biashara yao. 

Mafuta mazuri kabisa ni yale yenye OMEGA 3 ambayo ni pamoja na mafuta ya nazi, mafuta ya mawese, mafuta ya mbegu za maboga, mafuta ya ufuta, mafuta ya parachichi, mafuta ya zeituni na mafuta ya samaki

Imehaririwa mara ya mwisho 28 May, 2019 Saa 12:32 pm

Post a Comment

0 Comments