JE, WAJUA KUWA NDEGE HAZIRUHUSIWI KUPITA JUU YA NYUMBA YA MESSI??

Hii haitokei dunia kote lakini fahamu kuwa fanya ufanyavyo kamwe huwezi kupita na ndege juu ya nyumba ya mchezaji bora kabisa duniani wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi.

Zipo baadhi ya sehemu duniani ndege kamwe haziruhusiwi kupita ambapo kwa kimombo wanaita ‘flight restriction zone’ na baadhi yake ni kama Washington, D.C. Mecca nchini Saud Arabia na baadhi ya maeneo nchini Malaysia.

Hivyo basi ndege kutoruhusiwa kupita kwenye anga hiyo kamwe hakuhusiani na uwepo wa mchezaji huyo maarufu duniani bali ni kutokana na sheria ambazo zimewekwa, ndege kutopita maeneo hayo ambayo ni Gava Mar, Viladecans na Castelldefels yaliopo karibu na fukwe za bahari ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Lionel Messi huishi kwenye halmasahauri ya Castelldefels jijini Barcelona nchini Hispania na ndege haziwezi kupita kwenye maene yake ni kutokana na sababu hizo za kimazingira kwa mujibu wa sheria za Barcelona.

Eneo hili la Castelldefels hulindwa zaidi katika kuhakikisha linatunzwa mazingira yake kwakuwa lina uoto mwingi wa asili na hivyo kupelekea sheria za jiji la Barcelona kupiga marufuku ndege, kwasababu husababisha uchafuzi wa mazingira (Noise pollution) kwa viumbe hai wa porini wanaopatikana maeneo hayo.

Kwenye maeneo hayo ndege haziruhusiwi kabisa kupita pembezoni mwa fukwe za bahari mahala ambapo nyumba ya Messi pamoja na watu wengine maarufu wanaishi na sheria hiyo huwasaidia yeye na mastaa wengi mahala hapo kutobuguziwa na makelele ya ndege kupita angani ambapo ni kilomita 10 kufikia uwanja ulipo.

Post a Comment

0 Comments