JE, UNATAKA KUISHI MAISHA YA FURAHA NA UTULIVU? FANYA HAYA


1. Anza kuwaza vizuri, achana na mawo yanayoumiza hisia weka uzingativu kwenye mambo yanayokupa faraja na yenye kukupa ari ya kujilrtea mandeleo

2. Ondokana na hofu za maisha kwani changamoto ni sehemu ya maisha, ukweli ni kwamba kila chngamoto inayotujia tayari tunayo suluhu na kama hatuna suluhu ya changamoto hiyo basi isingekuja kwetu, utulivu na kuwaza vizuri ni mwanzo mzuri wa kupata majibu ya changamoto zinazotukabili

3. Safisha akili na moyo wako kwa kuandika kurasa tatu za chochote kinachokatiza mawazoni mwako wakati ulipoamka. Kuna kitu wenzetu wanaita MORNING PAGES

Nitaeleza kwa kifupi;


Morning pages ni kitendo cha kuandika kitu chochote kinachopita mawazoni mwako asubuhi unapoamka, siyo lazima kuandika karatari kubwa ya A4, lakini karatasi ndogo tatu ambazo unaweza kuandika kila kinachopita mawazoni mwako.

Iwe ni kitu ulikuwa unataka kufanya ndoto uliyoota usiku kitu ulichopanga kufanya ukasahau au jambo lolote linalopita mawazoni mwako hata mziki unaousikia mawazoni mwako, labda uliusikia usiku au siku iliyopita na ukaendelea kubaki mawazoni mwako.

Mwanautambuzi aliyetamblisha hii nadharia Julia Cameron anatanabahisha kwamba kama vile mtu unavyoamka asubuhi na kisha kuoga na kujiikia vizuri basi Morning Pages ni kama kuogesha moyo akili na hisia na hivyo kusikia vizuri na kuandaa moyo akili na mwili kupokea kitu kipya.

''Morning pages are three pages of writing (long hand) anything that comes to your head. Julia Cameron suggests that you make Morning Pages a practice that you keep every day while you are working through The Artist's Way, and hopefully, beyond.

The point to Morning Pages isn't to write incredible, novel-quality prose. The writing you do in your Morning Pages may not even be suitable for a letter to a friend! It's the little bits and pieces that run around in your head out of control. The words may not even piece together into full sentences. What you write doesn't have to make sense to any person on the face of the planet -- or even to yourself a few days later.

I compare Morning Pages to my morning shower. While I'm not visually dirty in the morning, I feel refreshed and ready for my day after taking a shower. Your shower takes care of your body. Morning Pages is a shower for your heart, mind, and soul.

There's no visible "dirt," but there might be something under the surface that needs attention. Or maybe a dream or two looking for a place to land. Or maybe a list of things you want to get done during the day. Or just random thoughts that plague you like a song you can't get out of your head.''

4. Tenda wema kwa wengine, tembelea wagojwa, fariji wenye matatizo au ta ushauri kwa wenye kuhitaji. kwa kutenda wema kwa wengine kutakufanya ujisikie vizuri.

5. Fanya tahajudi (Meditation) kwa dakika tano kila uamkapo. huhitaji kujifungia kwenye chumba na mishumaa, la hasha, unaweza kufanya tahajudi kabla ya kuwasha gari, chumbani kwako kabla ya kuondoka, kwenye daladala bila kujali kelele za abiria wengine, au ofisini kwenye desk lako. dakika tano za tahajudi kila siku zitakufanya uone tofauti

6. Angalia vipindi vya luninga vitakavyokufanya ujifunze jambo lakini pia kufuatilia habari za watu wenye kukuvutia na kutamani uwe kama wao ni jambo jema. Pia kukutana na watu wenye kukuvutia mpaka unatamani kuwa kama wao ni jambo jema pia.

7. Kusikiliza miziki uipendayo kila unapopata fursa ya kufanya hivyo ni jambo lenye kuleta amani na furaha moyoni.

8. Cheza mziki kama vile hakuna mtu anayekuona, kuna wakati unaweza kusikia mziki ukatamani kucheza lakini ukashindwa kutokana na mazingira. kama ukipata nafasi nyumbani kwako, jifungie cheza mziki kadiri unavyojisikia mpaka utosheke.....

9. Tafuta eneo tulivu lenye mandhari nzuri ya uoto wa asili uwe peke yako kwa ajili ya kuifanya akili, moyo na hisia kujisikia vizuri. sehemu zenye chem chem ya maji, uoto wa asili miti na milio ya ndege inafanya akili itulie.......

10. Mazoezi na mziki si kwamba ni faida kwa afya ya mwili pekee bali pia kwa afya ya akili. kukimbia au kutembea kilomita tano kwa siku kunaleta tofauti kubwa sana. Anza sasa...

11. Kumpigia simu rafiki na kuwa na mazungumzo yenye kuchangamsha, inaweza ikawa mnajadili jambo lolote litakalozua ubishani au mada yoyote kuhusu maisha au siasa. lakini pia wapo marafiki ulisoma nao wale marafiki wenye dhihaka (Comedy) ambao walilifanya darasa lichangamke ni vyema kuwakumbuka kwa kuwapigia simu ili kukuushana ya zamani na kucheka kidogo.


Post a Comment

0 Comments