JAMANI MKE WANGU ANANIZIDI AKILI NA MBINU, KUTWA YUPO KWENYE SOCIAL MEDIA


Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo.

Mke wangu sasa ananizidi akili na mbinu.

Nilimnunulia smartphone ya bei kama laki 7 aina ya Samsung, yapata miezi minne sasa tangu awe nayo.

Kinachoniumiza sasa hivi kazi zote ni mschana wa kazi.

Yeye hapiki, hapigi deki na hafui, muda wote yuko bize na simu yake.

Pia amejiunga social networks zote kama twitter, badoo, facebook, whatsapp, tango, we chat na instagram na nikitaka kupigana naye basi nimuombe pasword zake, hapo yupo tayari kurusha ngumi.

Usiku analala saa saba na akichelewa ni saa 6 usiku.

Yupo bize. nampenda sana na nahofia kumpoteza. Jamani nifanyeje? Vita nyingne ni pale anapoishiwa pesa ya bando, yani anadai pesa ya vocha kwa lazima mpaka nitaitoa.

Mitandao yote aweweka profile picture nzuri na tena Mungu alimjalia uzuri kama kabla lake Wairaq (wambulu) walivyo.

Anapotaka kubadilisha profile picture hapo ndo naumiaga zaid sababu anajimek up na kutoa nguo zaidi ya 5 na anavaa moja moja huku msichana wa kazi anampiga picha tofauti tofauti na yeye huangalia ile aliyopendeza.

Post a Comment

0 Comments