Kuna dalili mbalimbali ambazo zitakuonyesha kuwa mpenzi wako hataki kuendelea kuwa na wewe katika mahusiano.
Kuna baadhi wanaonyeshwa hizo dalili lakini wamo wanang’ang’ani kupendwa jambo ambalo utakuwa unajidanganya ndugu yangu.
Penzi likichuja hata ujibembeleze vipi ni sawa na kutuanga maji katika kinu huwezi kulirudisha.
Dalili ambazo utazijua kama umeachwa katika penzi jambo la kwanza atapunguza kukupenda kama ilivyokuwa awali.
Yale mapenzi aliyokuwa anakuapati yatapungua na hana muda na wewe tena.
Ukiona mwanaume wako hana muda na wewe hata hakuthamini kama ilivyokawa zamani jua hapo umeachwa.
Mwanaume anayekupenda kwa dhati lazima akujali na kukuthamini ukiona hayo mambo hayapo jua ndio umeachwa usisubirie kutumiwa SMS ya kuachana.
Pia kuna hili jambo jingine la mawasiliano ukiona mawasiliano yamepungua kwa siku anza kujitathimini.
Siku inapita hata huulizwi umeamkaje ama umeshindaje jua ndio dalili zenyewe hizo za kuachwa.
Haiwezekani kwa anayekupenda kupita hata masaa mawili hajawasiliana na wewe hata kama alikuwa bize namna gani lazima hata anavyokwenda kupata chakula cha mchana atakutafuta.
Lakini kuna wengine watapiga simu weeeeeee haipokelewi inakuja kupokelewa siku ya pili tena atajifanya hata hakuna simu yako huku wewe ukiwa unapatwa maumivu ya kimapenzi.
Hivi kweli mpenzi wako akupigie simu unakuja kumjibu siku ya tatu hapo ndugu yangu hakuna mapenzi anza kuchapa lapa mapema kabla ya jua kuzama kwa nini uendelee kupata maumivu kwa mtu ambaye hata hakufikirii.
Kuna mwanaume wengine wanasingizia kazi zinawabana hivi kazi hiyo inakubana unashindwa hata kutuma sms hata moja kwa siku ina maana unakosa hata muda wa kwenda kupata chakula ambapo muda huo huutumia hata kuwasiliana na mpenzi wako.
Jiulize tu hizo kazi zinambana hadi anapofika nyumbani ina maana hapati hata muda wa kulala kwa hiyo hata kuoga haogi hapana tusidanganyani jamani ina maana hashike simu akifika nyumbani wakati kutwa nzima unamuona online.
Mapenzi ni kitu kingine jamani kwa wale wenye mapenzi ya kweli wananielewa vizuri unayempenda hutamani siku isipite hamjaonana au masaa yasipite bila kuwasiliana.
Unakuwa na mwanaume ambaye anakutafuta siku ambayo yeye ana shida zake alafu unajihesabu una mpenzi. Hapo ni kujishushia thamani yako anayekupenda hawezi kukuchukulia wewe ni kama kidemu cha mzinga yaani yeye ndio akutafute.
Jambo jingine la kugundua kama umeachwa utaona mambo yake anafanya kwa usiri awali alikuwa anakumbia lakini utaona anaanza kukuficha.
Ukiona unafichwa baadhi ya vitu hataki ujue hapo ujue umeachwa. Anayekupenda hawezi kukuficha atakuwa muwazi kwako.
Ni muhimu ukayajua mahusiano yako vizuri na mtu wako kuliko kuendelea kupoteza muda kwa mtu ambaye hajakuweka katika akili yake.
Kuna vitu unaweza kuvilazimisha lakini sio kumlazimisha mtu akuweke moyoni.
Chukua maamuzi mapema ukiona mwanamke ama mwanaume ana dalili hizo anza kujipanga na kuangalia ustaarabu mwingine .
0 Comments