AMBER LULU AFUNGUKA KUHUSU KUCHEZA VIDEO ZA UTUPU

NA EMMANUEL MBATILO

Baada ya maneno mengi kuzagaa mtandaoni kuhusu msanii bongo fleva, Amber lulu kutakiwa kucheza video za utupu, amefunguka na kudai yakwamba ni kweli alifuatwa lakini hakupenda kufanya kazi hiyo.

Msanii huyo ambaye alijipatia umaalufu mkubwa kwa kupiga picha za nusu utupu amekaririwa akisema kwamba kweli alifuatwa na kutakiwa kucheza video hizo ili alipwe lakini hakuweza kufanya hivyo kwani aliona kuwa atamkosea mungu.

“Sisi ni binadamu, unakuwa unafanywa au unable stress unaweza kujikuta unafanya vitu bila wewe kupenda, sasa kile kitu mtu anakuletea mezani utie sahihi, unakuta hatujapenda, lakini we do, ikitokea nimefanya ni sijapenda na sio kwa ridhaa yangu”.

Post a Comment

0 Comments