Dunia imebadilika na idadi ya wanaovaa extra size imeongezeka, ukubwa wa khanga umebakia ule ule.
Unanunua khanga hata bila kuikata unapinda zote mbili lakini bado ni ndogo. Mbona vitenge tunauziwa piece tatu? Wenzenu walishaona umuhimu wa super size.
Kuna mitandio inatoka Karachi Pakistan, huwa na ukubwa wa kuridhisha, kama khanga zingekuwa size ile ingependeza.
Wekeni khanga za vipande vitatu, sisi mabonge tutanunua, soko la sasa hivi halikidhi mahitaji yetu.
0 Comments