Achana nae .. Unalala, haupati usingizi juu ya mtu ambae huenda amelala na mtu mwingine muda huu kwa amani tele.
Achana nae!
Unaangalia simu yako sasa hivi ukisubiri text ya mtu ambae unamuona yuko online anachati na mtu mwingine kwa furaha zote.. Achana nae!
Unaweka status za huzuni WatsApp kuonesha namna gani unavyoumizwa, wakati yeye yuko busy anamfikiria mtu mwingine, anampa furaha mtu mwingine, anamuweka status kuwa anampenda sana na wewe amekuficha usiweze kuiona status.
Achana nae..! Kweli unalia juu ya mtu ambae anamfurahisha mwingine?? Sio sawa bhana, hebu sikiliza, kama wewe sie ambae anakujali, basi hutakiwi kuwa na wasiwasi tena, wewe sie wake. Yuko mtu mwingine badala yako.
Ni ngumu, inauma sana na sio rahisi lakini kaza moyo, vaa moyo wa ujasiri, na hebu achana nae!! Ipo siku, utakuja kuwa na mtu atakaekusahaulisha magumu yote uliyopitia!!
0 Comments