Ni kweli sifa kuu ya mwanaume ni kumtunza mke wake na watoto,lakini mwanamke pia anatakiwa kumsaidia mpenzi wake mambo yakikwama, Dunia ya sasa imebadilika.
Ni hivi
Nimekuwa na mahusiano na huyu dada kwa miaka mitatu sasa ni binti mzuri kitabia ananipenda na sio mgomvi, lakini karibuni nitamuacha sababu ni mtu mbinafsi na bahili
Nilimkuta hana kazi nikamtafutia kazi lakini hata nikiumwa hawezi hata kuniletea machungwa, ni mwanamke anaependa mimi kumcare lakini yeye huwa hanijali mimi napokwama, yaani ni mwanamke wa kwenye raha tu
Nikimtishia kumuacha mara nyingine huwa anataka kujiuwa inanibidi nipretend tu kuwa mapenzi yetu yana uhai, lakini nataka kumuacha kimya kimya, mwanamke mbinafsi nikiowa itakuja kuniletea shida, nikipata hata majanga najua na ndoa ndio itakuwa imekufa
Kuowa mwanamke mbinafi asiyeweza kujitoa kwako, ni kujiletea majanga ya baadae, mwanamke bahili kwa dunia ya sasa ni janga, ukiowa jihesabie maumivu
0 Comments