Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Ray C amedai kuwa anajihisi mnyonge na anaonelea ni vema ajitoe uhai ili akapumzike
Kupitia jumbe kadhaa za kutatanisha alizozichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ray C alisema yuko na mawazo mengi ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda.
" Mwaka huu nahisi kama nitajiua, nina mawazo mengi sana," Ray C aliandika Instagram.
Kwa upesi wafuasi wake, waliingilia kati na kutaka mwanamuziki huyo atafute ushauri badala ya kuchukua hatua hiyo.
Hata hivyo, wengine walidai, Ray C yuko na mazoea ya kutishia kujitoa uhai, mbinu waliodai yeye hutumia kujitafutia umaarufu baada ya kudidimia kimziki.
Ray C aliwahi pelekwa katika kituo cha kurekebishia tabia baada ya kuathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya.
0 Comments