HAYA NDIYO MAMBO MAKUU 3 YANAYOVUNJA NDOA

Uko sahihi kabisa na hayo matatu yanaingiliana katika kuchagiza au kuiweka chali ndoa.

Pesa inaweza kuimarisha ndoa endapo tu mwanamme unatimiza wajibu wako yaani kila kitu unakikabili kifedha hata kama mke nae anafanya kazi.

Kumbuka pamoja na kuoa wapo wazazi wa pande zote mbili ndugu wa pande zote mbili, hivyo kama uko kawaida basi ndoa itatulia na kila mmoja atakua hasumbui.

Ukiwa na uwezo yaani pesa, basi utagombaniwa na pande zote nne mkeo ,watoto, wazazi na ndugu na ukitimiliza basi hakutakuwa na vijimaneno, ukishindwa basi kelele zitaanza kupitia mkeo.

Tendo la ndoa halina tatizo sana na ni wote wawili mkiwa na tamaa ya ngono basi mtalihalalisa mme kwa mchepuko, na mama kwa kijana mdogo.

Ila tendo la ndoa laweza kuyumba kwelikweli kama mme hana uwezo wa pesa na kuna mtu pembeni afanya uchambuzi yakinifu khasa kama mke umefahamu namna ya kuchagua.

Lakini kiukweli katika yote namba 1 ni kitu cha kwanza kabisa, kwasababu kitatoa tathmini ya hayo miwili ya chini.

Post a Comment

0 Comments