FAHAMU JINSI SIMU YAKO INAVYOWEZA KUSABABISHA MAUMIVU YA SHINGO / KICHWA

TEXT NECK SYNDROME
huambatana na 
1. Maumivu ya misuli ya shingo

2. Maumivu ya kichwa

3. Maumivu ya bega

4. Ganzi sehemu za mikono
endapo tatizo litapokuwa kubwa

CHANZO CHAKE
Mikao mibaya unapotumia simu na laptops

Kadri unavyoinamisha shingo kufuata simu yako au laptop unapoitumia unasababisha MISULI YA SHINGO(upper trapezius) kuelemewa na kushindwa kubeba uzito wa kichwa.

Hii hupelekea KUKAZA kwa misuli hyo(cervical spasm), kuchoka(fatigue) na kuleta MAUMIVU.

Maumivu haya hutokea mara kwa mara unapotumia simu au laptop au kusoma kitabu kwa MUDA MREFU . Pia hupelekea mtu kupata maumivu ya kichwa kama tatizo ni kubwa.

TAKWIMU
-Tatizo hili huwapata sana vijana kutokana na kuwa na matumizi makubwa ya smartphone na laptops

MATIBABU.
1- Weka simu sambamba na uso mbali kidogo na macho

2- Uisiinamishe shingo kuiangalia simu/ laptop kwa chini

3- Tumia laptop holder kurekebisha uwiano wa uso na laptop

4- Muone Daktari wa fiziotherapia kwa matibabu zaidi ya maumivu, ganzi na kuuma kichwa.

Kwa matibabu uchunguzi na tiba wasiliana nami 0718 22 48 40

Post a Comment

0 Comments