AIKA AFUNGUKA SUALA LA NDOA YAKE NA NAHREEL

Nyota kutoka katika kiwanda cha Bongo Fleva, Aika Mariale amewafungukia watu wanaowashauri wafunge ndoa na mzazi mwenzake Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ ambaye pia ni msanii wa kundi la NavyKenzo, akisema, kuwa na mapenzi ya dhati kwao ni zaidi ya ndoa.

Aika alisema, watu wanashindwa kuelewa kwamba ndoa ni hitimisho la matokeo ya mapenzi ya dhati ambayo kwao yapo, hivyo hawababaiki na ndoa.

“Unajua watu wanashindwa kuelewa mapenzi makubwa niliyonayo kwa Nahreel, maana hatushindwi kufunga ndoa hata kesho kama tukiamua, watu walijue hilo. Muhimu tuna amani na mapenzi ya kweli, hiyo inatosha na ina maana zaidi kwetu,” alisema Aika


(Visited 1 times, 1 visits today)

Post a Comment

0 Comments