Ndoa nyingi zimekuwa na migogoro kwa sababu wanandoa wengi wameingia bila kitambua nini anapaswa kufanya ili kuidumisha furaha ya ndoa yao wengi wetu tunatumia kigezo cha upendo tunasahau kama kuna mambo yamsingi nayamuhimu ambayo tunapaswa kuyatekeleza ili kuidumisha upendo na amani kwenye ndoa zetu.yafuatayo ni mambo ambayo wanandoa wanapaswa kuyafanya ili yakutengeneza familia bora na yenye amani.
1: KUTAMBUA THAMANI YA MWENZAKE.
Katika familia kila mtu anapaswa kutambua thamani ya mwenzake hii husaidia kila mtu kuona mwenzake anaumuhimu mkubwa sana kwake nakatika kujenga familia yao kama ujuavyo kitu chochote unachokithamini kazima ukipende kwa moyo wako wote kwahiyo thamani hudumisha upendo.
2: KILA MTU KUTAMBUA NAFASI ALIYONAYO KATIKA FAMILIA.
Katika familia kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake kikamilifu ikiwa ni mwanamke unapaswa kujua kuwa wewe ni mama unapaswa kuyatimiza majukumu yako kama mke na kama mama hakikisha majukumu yote yaliyo ndani yauwezo wako unayafanya kikamilifu pia unapaswa kuwa mstali wa mbele kuulinda upendo na kuidumisha furaha ya mumeo. Vilevile mwanaume pia anapaswa kusimama kwenye nafasi yake kikamilifu pamoja nakusaidiwa majukumu na mwanamke ila bado anamajukumu mazito katika familia hivyo lazima ayatekekeze kikamilifu pia lazima asimame kidete kuimarisha amani na upendo katika familia.
3: KUJIHESHIMU, KUMUHESHIMU MWENZAKE NA KUWAHESHIMU WENGINE.
Hakuna kitu kitamu jamani kwenye ndoa kama ukijua mwenzako anakuheshimu yani utajiona ni mtu flani ivi tofauti na mwingine tena utahisi ulichelewa kumpata mkeo au mumeo. Heshima ni jambo la msingi sana kwanza kila mwanandoa anapaswa kujiheshimu yeye mwenyewe akijiheshimu lazima kila utakachokifanya kamwe hawezi kumkwaza mpenziwe pia anapaswa kukuheshimu mume/ mke wake wapendwa heshima ni duru ya ndoa mheshimu mwenzako uone yani utafurahi mwenyewe,pia msiishie kuheshimiana wenyewe tu pia mnapaswa kuwaheshimu na wengine hii huleta sifa njema katika familia kwahiyo wahenga walisema HESHIMU UHESHIMIKE.
4: UKWELI NA UWAZI.
Ndoa nyingi zina migogoro kwa kukosa ukweli na uwazi na jambo hili husababishwa na kila mtu kutokumuamini mwenzake jamani wanandoa acheni kufichana sio vizuri ebu kuweni wawanzi kwa wenzi wenu kufichana si kumaliza tatizo bali kuongeza tatizo ivi unapomficha siku akijua ukweli unahisi kunauoendo tena hapo!? Lahasha utakuwa umezalisha ugomvi usioisha hautoaminika tena hata ufanyeje. Kuna mtu mwingine hatakama anamtoto nje haseni kwakuogopa kuachwa anasahau kuwa dunia haina siri ipo siku atajua tu niheri umwambie mapema wewe mwenyewe kuliko kuja kusikia kwa mtu baki huwa ni hatari zaidi! Hivyo basi uwazi nimuhimu jaribu kumsirikisha mwenzako kwa kila jambo mnapoishi pamoja ninyi niwamoja.
5: KUPENDA NDUGU PANZE ZOTE.
Hii pia huwa nitatizo lingine kuna baadhi ya mwanandoa wanabagua ndugu yani anapenda wakwake tu kwamwenzake anawaona mzigo acheni kabisa tabia hii! Ndugu wote wa mume/mke wanathamani sawa usibague kama nikisaidia saidieni wote bila ubaguzi hii inasaidia sana kuleta amani na upendo katika familia acheni ubaguzi wajali na kuwapenda wote.
6: KUFANYA KAZI KWA BIDII KWA MANUFAA YA FAMILIA.
Kila mwana ndoa anapaswa kufanya kazi kwabidii kuinua uchumi wa familia yao hii husaidia sana kuboresha maisha yao kwa ujumla katika utafutaji wa familia si swala la mwanamke au mwanaume peke yake wote wanawajibu wakuchakarika ili kusaidiana majukumu ya familia kwenye hili wapendwa hakuna kutegeana NGUVU MOJA SAUTI YAUSHINDI UVIVU MWIKO.
MWISHO.
YOTE HAYA KWAUJUMLA WAKE YAKITIMIZWA BASI NDOA ITAKUA NA FURAHA NA AMANI SIKU ZITE. MAPENZI HAYANA UCHAWI!
0 Comments