Wapenzi wasomaji wa makala zangu Leo nataka kuzungumza na wanawake jinsi wanavyoweza kuwadibiti waume / wapenzi wao wasichepuke au hata kuwaza kufikiria mchepuko .jamani hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke hasa anapogundua amepata uaridi yaani mwanamke aliekamikila kila idara msikivu,mvumilivu,anaheshim,mpole,anajituma,mkarimu n.k.
Yapo mambo ambayo mwanamke akiyafanya basi kusalitiwa na kufumania atasikia kwa jirani kwake Hakiwezi kutokea kitu kama hicho niupendo tu siku zote hakuna maumivu, baadhi ya mambo hayo ni:.
1: HESHIMA.
Mwanamke anaejitambua lazima amheshimu mume/mpenzi wake siku zite heshima inaambatana na utii hata maandiko ya dini yanasema mwanamke amtii mume na mume ampende mke,jamani muwaheshimu waume zenu kama kweli kama kweli ulikubali kuanzisha mahusiano basi ulimpenda kwa dhati hukulazimishwa basi mpe nafasi yake aone kama hakukosea kuchagua, kunawanawake jamani mnawafanya wanaume wajute kuwatafuta maana nikisirani moja kwa moja ndani hajulikani mwanamke nani na mwanaume nani hii sio haki wanawake badilikeni.
2: ZUNGUMZA MANENO MATAMU KILA WAKATI.
Mwanamke kauli jamani, ulimi ukiutumia vizuri hutoa maneno matamu zaidi ya asali!, ebu kila wakati jifunze kuzungumza maneno matamu namwenzi wako , akikukosea usitafute sababu yakukwepa kosa mfuate tu mwambie,"Baby,dear,honey,My love, my husband nimekosea NISAMEHE sitarudia tena nakuabudu," kauli hii hatakama mwanaume alichukia kiasi gani azima hasira ziishe utasikia anamwambia,"unajua baby mm nakupenda ila unapenda kuniuzi mimi sitaki bwana", muda huo kakukumbatia ebu niambie kunaugomvi tena hapo!? Hakuna.
Pia jifunze kumpa pole nakumtia moyo pale unapohisi amechoka au amefadhaika kwa namna moja ama nyingine, wanaume nikama watoto, mtoto hata kama ameumia kiasi gani akisikia neno pole tu ananyamaza hapohapo ndivyo mwanaume anapaswa kulelewa.
Usisahau KUSHUKURU kwa bila jambo zuri analikufanyia au kwa zawadi au kitu chochote anavhokuletea hii itamfanya ajue kuwe unaithamini upendo wake na kila anachokifanya kwako unakithamini.
Mwisho usichoke kumtamkia neno NAKUPENDA kila wakati hii itamfanya asikusahau kila aendapo lazima akukumbuke wewe tu sangapi atapata muda wakuwaza mchepuko!? Hawezi.
3: USAFI.
Mwanamke usafi bibi! Wanaume sikuzote wanapenda mwanamke msafi utatambulishwa wewe kila sehemu mnapoenda tena mnatembea mmeongozana hakuna mtu anaependa kuishi na mtu mchafu.swala hili la usafi nazungumzia pande zote yaani usafi wa mwili mavazi na mazingira kwaujumla. Kunawanawake niwachafu jamani hajijali yeye wala mahali anapokaa, kuoga shida, kufua matatizo, nyumba usisema kikombe juu ya tv,viatu kwenye sofa, sufuria kitandani yani humo ndani ni tafrani hapaeleweki sangapi mwanaume atakukumbuka au kutamani kurudi nyumbani mapema hapo mwenyewe unampa nafasi yakutafuta pakupumzikia.
Wanawake ebu badilikeni jamani usafi nimujimu sana! Jitahidi usafi binafsi, nyumbana mazingira kwa ujumla japo itakuwa umemshika atoke aende wapi kutwa yuko pembeni atoke aende wapi? Yani kama amelogwa.
4: MAPISHI.
Mwanamke jiko, mwanamke yeyote lazima ajue kulitawala jiko apike chakula kitamu na chenye radha, hakuna kitu kizur kama mwanaume akila chakula kitamu tena kimepikwa na mwanamke anaempenda yaani hujisikia fahari sana mwanamke niwajibu wako kujua mume anapenda chakula gani ili iwe unamuandalia kwa umahiri sio kila siku hotelini wakati mwanamke upo hapo mama unatafuta kuachwa au kutafutiwa msaidizi wanawake badilikeni.
5: MUITE MUME/ MPENZI WAKO MAJINA MAZURI YA MAHABA KILA WAKAT.
Hata namna unavyomuita jina mwenzi wako kunamuongezea hali flani ivi ya kupenda nakutamani kuwa na wewe muda wote, lakini mwanaume unamuita unamuita ovyoovyo mpaka kero, ebu jaribu kumuona majina yamahaba uone utakuwa umemloga kweli nakwambia! Mf: hubby, dear,sweet, honey, n.k ikiwezikana hata jina lake kama unaweza kuliita kwamahaba bibi liite nayo inapendeza pia.
Epuka kumuita jina mwanaume kwakuanza na WE flani aaaa! Hapo umepotea nidharau kubwa sana kwa mwanaume anaejitambua haitiki.
Hayo ni mambo makuu matano ambayo husaidia kwa 90% mwanaume asichepuke wala kuwaza mchepuko mambo haya ni uchawi tosha kwa mpenzi wako.
Ebu jaribu alafu ulete mrejesho hapa.
Asante!
0 Comments