DAR – Nimejiunga na mitandao ya kijamii (yani Facebook, Instagram na Twitter) zamani kiasi kwa jina langu halisi @Fredymasolwa, nimeona faida na hasara zake lakini mpaka sasa faida za kutumia jina halisi ni kubwa sana kuliko hasara.
Kama kukutana na watu wengi niliopotezana nao kitambo wenye faida katika maisha yangu, pili kupokea mafundisho, maono na maoni mbalimbali ya kimaisha n.k, tatu kupanua wigo mkubwa wa kifursa, elimu na kazi toka kwa watu, nne kutafutwa na watu makini kifursa kwa kuwaandalia mipango biashara, ushauri wa kodi, kisheria, kazi na nyaraka kazi za Taasisi zao, NGO n.k
Tano kupata marafiki, ndugu na jamaa wenye msaada kwangu siku zote, lakini ingawa hasara zake zipo chache sana, kwani mimi ni Baba Eliza, Eva na mme wa Faith anayenipa raha duniani, teh teh!
JINA FEKI
Siku moja kulikuwa na uhitaji mkubwa sana wa Mwanamama machachali, mtangazaji wa radio Magic FM ya Jijini Dar es Salaam na MC wa sherehe mbalimbali “Mishi Bomba”, nilipigiwa simu na mtu mmoja akidhani nafahamiana naye, kwani mimi nafanya shunguli za MC kupitia kampuni ya Fede Burudani Ltd _(Karibuni sana Music na MC Tsh 490,000 tu, kwa ofa piga 0767-011406)_.
Nilishindwa kumpata haraka na kabisa, kwani nilijaribu kutafuta namba yake ya simu bila mafanikio, niliingia kwenye mitandao ya kijamii yote sikupata jina lake halisi la Mwanahamisi wala la kazi, niliambulia majina kama Mish B, BombaMishi, Mishibombaxyz, Mishi Bomba n.k na kushindwa kuelewa lipi ni sahihi.
Kwani watu hawa walimtaka sana kwa shunguli ya “Kitchen Party” na mpaka kufikia Mwanahamisi kukosa fursa hii, kumbe anatumia jina la Mishie Bomba, unaweza tazama yeye ujihita Mishi Bomba au Mishi B lakini kwenye mitandao anatumia Mishie Bomba.
Hasara ni nyingi sana, unakuta mtu anajina zuri kabisa lakini, anajihita Mashaka jzatada, mara Maulidxyazagatakuacak Mpamile, utakuta Joseph Mandala kwasababu ni shabiki wa Arsenal anajiita Joseph Arsenal, mara Kana Katafunua wakati yeye ni Bahati, Hadija Makoye anajiita Hadija Yanga.
Fredy Mashikolo anajiita Fredhinyo Xyaza, mara mtu anakuja na swaga za Xy_wcb, mara Zy_Darasa, nampenda sana James Tupatupa wa Clouds Media na ninamshanga sana Mtangazaji wa Clouds Media anajihita “Cotinyo” wakati sio jina lake, ni fujo tu mara huyu naye MuhikwXYmatthew, mara Obama wa Bongo, Ibrah Majanga na majina mbalimbali wakizani wanaifungulia Dunia.
Nimetafakari sana sababu za kuandika majina feki sikupata jibu sahihi, labda …sijui ni ujana au uzee, kutojua, makudhi, mahaba, au kudhani wanaenda na wakati.
FAIDA YA JINA FEKI
Kuna jina kama Mzee Mwanakijiji (M.M.M) hii ni “Brand and Products” kwa jicho langu la nne, kuna haja sasa mkuu huyu kutumia akaunti hii kifursa na kibiashara mwaka huu kutengeneza maandishi yake kwenye Vitabu, Majarada na Maandiko makubwa na mambo mengine mazuri kwa faida. Kwani jina lake ni feki lakini lina taswira za kifaida sana.
Lakini kama mtu unatumia jina sahihi la kibiashara nje na lako la kiserikari kwenye akaunti zako, hii ni fursa sahihi sana mfano Happy Fashion Shop, Segere Investment, MC Kazaura, Maulid online shop, Ndetyia Bar, Mchama Kuku Poa n.k
Hapo kuna hasara chanya kwa upande wa pili, lakini kuna faida ya kutangaza biashara yako na kukuza kipato na mtaji wa biashara yako, kuongeza idadi ya wateja wako, kutumia ukuta wako kwa matangazo mbalimbali toka sehemu nyingine, kutumika kifursa au masoko na makampuni hasimu kwa kukandamiza kampuni jingine kimasoko n.k bila kuvunja sheria za nchi, kufundisha watu na mambo mazuri kwako.
HASARA YA JINA FEKI
1. Kukosa heshima kwa post zako, na kuonekana na heshima kwa watu wenye akili sawa na wewe, bila faida kimapato na maisha
2. Kukosa fursa za kikazi, biashara, elimu na mambo mbalimbali, kwani haya yote utokana na maombi, mtu anaweza kukupa taarifa kwa haraka juu ya kazi na hana mawasiliano yako, lakini kama unajina sahihi labda facebook ni rahisi kupatikana
3. Kukosa ndugu na jamaa uliopotezana nao miaka mingi, kwani wanaweza kuwa msaada kwako kwa hali yako ya sasa.
4. Kuandika ujinga wenye comments nyingi, zenye kufanya kushinda muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii na kushindwa kuongeza kipato, kufanyakazi sawasawa, kuchelewa kulala n.k
5. Kukosa uaminifu kwenye jamii inayokusoma kwenye mitandao wa kijamii, na kukosa fursa za kazi, elimu na fursa pale zinapotokea kwani mtu uchukua muda kukujua.
Na mambo mengi yenye mitazamo ya kielimu, taarifa sahihi, biashara, kazi, mapato mapya na mambo mengi.
Mfano mzuri ni Oscar Oscar wa Efm ametokea Facebook na kuonekana ni mtangazaji na mchambuzi sahihi wa michezo sasa.
NIKIKUMBUKA NALIA.
Kuna rafiki yangu anaitwa Coletha Joseph nilisoma naye shule ya sekondari, nilikutana naye kitambo kidogo na kuniambia alisoma Ugavi, lakin kwa uharaka tuliokutana naye na furaha iliyokuwepo tulishindwa kupeana mawasiliano ya simu kisha kuachana, nilirudi kuendelea na majukumu yangu Dar yeye nikimuacha Mwanza.
Siku moja kulitokea kazi ya kumtaka Afisa Ugavi Daraja la chini wenye sifa kama za Coletha, nikamkumbuka na kuanza kumtafuta kwenye mitandao ya kijamii kwani sikuwa na simu yake, sikufanikiwa hili nimpatie hili dili la kazi ya Ugavi.
Majuzi nimemuona tena Mwanza miaka mingi ikipita akiwa na hali sio nzuri kimapato na maisha, nikamuuliza anatumia jina gani kwenye mitandao ya kijamii, akasema Colexmbiseee na madudu kibao mbele mbise akiwa ndiye rafiki yake wa kiume, niliumia sana na kucheka kama Christian Bella kimoyo.
Naona Colex wa facebook akikosa fursa, akikosa mtandao wa watu aliosoma nao zamani wenye nafasi kwenye maTaasisi, kampuni na ofisi kubwa na mambo mazuri kwake.
Tutafakari pamoja sasa, kupitia kitabu cha Jossey Bass (2013) ” The Seven Success Factors of Social Media Business Strategies” utaona umuhimu wa kutumia jina sahihi kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii, kutumia base kubwa ya “followers” wako kujifaidisha kibiashara na kimapato kuliko kutumia kisifa kwa maisha ya kuigiza yatakayo kunyima faida.
Kama utashindwa kusoma kitabu hiki, basi unawezafata ushauri wa Ms. R. Kay Green, CEO wa RKG Marketing Solution akikwambia kujitaidi kufanya mambo matatu kwenye mitandao ya kijamii kwa faida kuliko hasara kama ” one – stop company yourself to others, two – stay true to your real self, and three – align your real self with your ideal self” utapata Muziki wa kucheza 2017 kupitia Mitandao ya Kijamii.
Mwisho!
0 Comments