Makosa yanayofanywa na wanaume katika mahusiano


Kuna mambo ambayo mtu anaweza kufanya pasi na kujua kuwa anafanya makosa. Ikija katika masuala ya mahusiano, wanaume wengine huchukulia kama mzaha. Wakishafaulu kutongoza na kumteka hisia mwanamke, wao hujisahau na kuanza kuishi nao kama mtu wa kawaida.

Leo tumekuja na ujuzi wa kukuonyesha makosa ambayo unaweza kuwa unayafanya bila kujua kuwa yana athari. Kiufupi ni makosa ya kijinga ambayo yanaweza kuepukika kirahisi iwapo utayafuatilia.
Hii ni muhimu kwa kuwa ukiachana na makosa haya basi unaweza kudumu katika mahusiano marefu na mpenzi wako zaidi.

Yafutayo ndiyo makosa yanayofanywa na wanaume katika mahusiano;

Unasahau kujijenga kibinafsi
Kosa lengine ambalo wanaume hujipata katika uhusiano ni pale ambapo wanatelekeza majukumu yao ya kujiendeleza kimaisha. Wanasahau mambo ambayo walikuwa wakifanya ama walikuwa wakitarajia kufanya kabla kuingia katika uhusiano wa kimapenzi.

Kusahau marafiki zako
Ni kawaida kupunguza mawasiliano na marafiki zako pindi ambapo utaingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke. Lakini hii haimaanishi kuwa hufai kuwasiliana nao kabisa. Marafiki zako watabaki kuwa marafiki zako. Mwanzo kabla kuingia katika mahusiano marafiki zako walikuwepo. kwahiyo swala hili usilipuuze kwa kuwa bado marafiki zako wako na umuhimu mkubwa katika maisha yako.

Kuacha kutimiza ndoto zako
Kama tulivyoeleza katika hoja ya pili, maisha hayaishi pindi utakapoingia katika mahusiano. Mahusiano kikawaida yako na yatazidi kuwapo. Usikatishe furaha ama ndoto zako. Kama ulikuwa una mipango ya kufanya jambo fulani katika maisha basi ni jukumu lako kuhakikisha kuwa ndoto hio inatimia.

Kuzama akili yote katika mahusiano
Kuna wanaume wengine wakiingia katika uhusiano na mwanamke basi wanajisahau kabisa. Maisha yao yote yanabadilika na kuzungukwa na mwanamke huyu. Wako tayari kufanya lolote au chochote kwa sababu ya huyu mwanamke. Hii si tabia nzuri kwa sababu huyu mwanamke hataenda mahali. Atakuwa na wewe muda mrefu hivyo hupaswi kufanyika kana kwamba huyo mwanamke ni kila kitu kwako.

Kuishi kwa mazoea.
Hii itatokea pale ambapo wewe na mpenzi wako mnaishi katika maisha ya kujirudia. Ni kama mumetengeneza ratiba ya kuyapeleka maisha yenu. Jumamosi hadi Ijumaa kuna ratiba ambayo munaifuata. Kuishi katika maisha kama haya kunaboesha na kuchosha. Mahusiano yenu hayana utofauti na vile mwaka jana ilivyokuwa. Mwanaume anapaswa kubadilisha mtindo huu.

Mfano anapaswa kumsaprize mwanamke na mambo tofauti tofauti ambayo hakuyatarajia.

Post a Comment

0 Comments