India: Mke Ajiua Baada ya Kudhihakiwa na Mumewe Kuhusu ngozi yake


Mwanamke mmoja nchini India mwenye miaka 21 anadaiwa kujiua kutokana na kudhalilishwa na mumewe kwa sababu ya rangi nyeusi ya ngozi yake.

Polisi wa jimbo la Rajasthan wamefungua kesi dhidi ya mume wa mwanamke huyo baada ya baba wa marehemu kumshutumu mume kuwa chanzo cha kifo cha binti yake.

Polisi wameiambia BBC India kuwa mwanaume huyo hajakamatwa. Na mume akiwa bado kutoa taarifa kuhusu shutuma dhidi yake.

Hii si mara ya kwanza kwa vitendo vya dhihaka dhidi ya wanawake wa India wenye rangi nyeusi kutokea na kusababisha vifo. Mwanamke mmoja mwenye miaka 29 alijiua mwaka 2014 baada ya mumewe kudhihaki rangi ya ngozi yake, polisi wameeleza.

Post a Comment

0 Comments