Shoga usipojitambua utasema umerogwa!


WANAKWAMBIA nazi nazi tu hata ivunjwe uile haiwezi kuwa embe, upo nyonyo? Heee heeeiya nashanga unavaa mini msibani kwenye sherehe unavaa kanga hadi usoni, inahu?  Kama ulikuwa hujui jua sasa, unashangaa poda ina unga  inatoa harufu wakati unga wenyewe hadi uingie maji ndiyo utoe hiyo harufu! Haloooo eeeeehhh! Mji leo umekuwa wa baridi kama barafu linalochanganywa kwenye kapu la samaki! Leo nipo na wewe shoga yangu unayejifanya umeshajifunza kwa kungwi wako lakini kwangu ndiyo kwanza mvua za vuli zimeanza, upo? Shoga ukitaka kujua uchungu wa kitanda chaga ivunjike!
Wapo walioolewa na wanaume wanaofanya kazi za kusafiri, pia wapo ambao waume zao hupendelea kusafiri pale wanapopata likizo ofisini kwao! Shosti, mumeo kama akisafiri andaa basi jinsi ya kumpokea ili ajue ulivyommisi, siyo anakuja anakutana na mambo yaleyale aliyoyaacha wakati anakwenda likizo.
Ngoja nikung’ate sikio likuume kidogo shosti wangu! Kama mumeo kaenda likizo yake ya kiofisi na wewe ndiyo wakati wako wa likizo ili wote mkikutana muwe wapya na stress zote mzitupilie mbali.
Kama bado hujajanjaruka nakusihi shosti wangu ujipange, ikibidi umtafute kungwi akufanyie masahihisho kwa yale uliyosahau au akupe maujuzi zaidi, nia kubwa ikiwa tu ni kuipa uhai ndoa yako.
Asikwambie mtu, kuna wakati ndoa inachosha kwa sababu ya kuonana kila siku, lakini mwenzako anaposafiri hujikuta unamkumbuka sana na kutamani arudi ili maisha yaendelee.
Ila kuna wanawake wengine huwa hawana muda na waume zao, anammisi lakini akirudi hata ile hali ya kummisi haioneshi anaongea naye kama vile walikuwa wote siku zote.
Shosti wangu, mume ukimuonesha mapenzi yaliyopitiliza, hawezi kukuacha na wakati huo ndiyo wakati wa kumuonesha kuwa unampenda, unaweza kumuandalia chakula kitamu ambacho anapenda kula, ambacho huwa unakipika kwa nadra ili aelewe umuhimu wa siku hiyo.
Muandalie nguo za kuvaa baada ya kuoga akitoka safari, hii siku inakuwa ni spesho kwani najua si kawaida ya wanawake wengi kuwaandalia waume zao nguo kwa sababu na wao wanachohisi, lakini siku hiyo ifanye spesho kwa kumuandalia na kama anarudi usiku, basi iwe nguo ya kulalia.
Yaani siku hiyo fanya vitu vipya kwake ambavyo vitakuwa kama sapraizi na baada ya hapo sasa muandae kwa faragha iwe ya uhakika, isije kuwa faragha kama aliyozoea siku zote, hiyo iwe ya ‘baby come back’ kama ulikuwa ukichokachoka, siku hiyo usichoke bibi kwani hata yeye huenda akajiuliza umechoshwa na nani na yeye hakuwepo.
Kwa leo niishie hapa shoga yangu. Tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi. Ni mimi Shangingi Mstaafu ukipenda niite Anti Naa au Anti Nasra!

Post a Comment

0 Comments