Maisha ya mwanadamu yanapitia changamoto nyingi sana hadi kufikia kilele cha mafanikio, changamoto hizo zinaweza kumfanya mwanadamu kukata tamaa na wakati mwingine kufikiria maamuzi magumu ya kujitoa uhai wake.
Asilimia 79 ya vifo hivyo vitokanavyo na watu kujiua hutokea katika nchi zenye uchumi wa chini na zenye uchumi wa kati.
Sababu zinazopelekea watu kuchukua uamuzi wa kujiua zikiwemo magonjwa ya akili yasiyotibiwa mapema, japokuwa mtaalamu wa magonjwa ya akili, Kay Redfield Jamison yeye anasema “Kila mtu anayejiua huwa na sababu zake mwenyewe: za kibinafsi, zisizojulikana, na zinazohangaisha.
Video: Haya ndiyo madhara ya msongo wa mawazo, Sonona ‘Kujiua’
Kwa mujibu wa gazeti la Mainichi Daily News robo tatu hivi ya watu wa umri wa makamo waliojiua kwa sababu ya matatizo yanayosababishwa na madeni, kufilisika kwa biashara, umaskini na kukosa kazi.
Matatizo ya familia pia yanaweza kuwafanya watu wajiue, Gazeti moja la Finland limeripoti kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa “wanaume wa umri wa makamo waliopata talaka kujiua.
Naye mwandishi maarufu wa Japan, Ryunosuke Akutagawa aliyeishi katika miaka ya mapema ya karne ya 20, aliamua kuandika baadhi ya maneno muda mfupi kabla ya kujiua akianza na maneno haya KUISHI ni kuteseka, kwa wazi, sitaki kufa, lakini…”.
Uchunguzi uliofanywa huko Hungaria ulifunua kwamba wasichana wengi wanaofikiria kujiua ni wale waliolelewa katika familia zilizovunjika.
Aidha, Mwezi Septemba umetengwa maalum kuhamasisha watu dhidi ya tatizo hili la watu kujiua.
Mwanasaikolojia ametoa ushauri kwa jamii kujihusisha sana kumcha Mungu na kuwaona wataalamu wa kisaikolojia inapobidi, ikiwa ni njia sahihi ya kuzuia kutokea kwa tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.
0 Comments