UKISIKIA familia yenye mambo, basi ni hii ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye dada yake, Esma Khan ameweka wazi kuwa mwanamke anayeleta mapenzi ya kizungu kwa kaka yao huyo wanamuondoa.
Esma ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, Diamond au Mondi kufika hapo alipo ni juhudi na maarifa yake pia wao kama familia wana mchango mkubwa kwake ndiyo maana mara nyingi walikuwa mstari wa mbele kumkumbusha mpaka siku ya shoo zake hata akisafiri, kwa hiyo hata suala la mwanamke lazima wampe ushauri.
“Unajua sisi huku kwetu uzungu wa mwanamke kutaka wajifungie tu ndani na kukumbatiana hatutaki na nilishasema akitokea wa hivyo tunamuundia kamati na mama Nasibu jinsi ya kumuondoa,” anasema Esma
0 Comments