WANAWAKE WA NYUMBA KUBWA IGENI KUTOKA NYUMBA NDOGO

Neno nyumba ndogo au nyumba kubwa si geni masikioni mwa wengi...

Mara nyingi nyumba kubwa inamaanisha Mke halali wa ndoa anayetambulika kifamilia na katika misingi ya kidini kama mlifunga ndoa kanisani au msikitini...pia endapo mlifunga ndoa ya kiserikali..

Nyumba ndogo inaweza ikatafsiriwa kama mke ambaye si halali, hatambuliki kidini wala kijamii bali ni mwanaume anaamua kutafuta kwa lengo la kukidhi haja zake ambazo huenda hatimiziwi vizuri na mke wa nyumba kubwa...

Nyumba ndogo imeonekana kuwa na nguvu sana kwa kuwakamata waume za watu wasifurukute, wasisikie la kuambiwa, yaani hapo ndiyo wanakuwa wamefika...wengi husema wamepewa limbwata...lakini mimi nasema hakuna limbwata wala nini, ni ufundi tu na ubunifu ambao nyumba ndogo anautumia..

Angalia hii...
1. Mapishi....nyumba ndogo mwanamume anaweza kupikiwa mapishi ya ufundi wa hali ya juu..chakula kikatengwa mezani kwa ufundi wa hali ya juu...lakini nyunba kunwa mke anapika michemsho michemsho kishaanatenga mezani ilimradi tu ametwnga..

2.Nyumba ndogo ukiingia unapikelewa na tabasamu mwanana lakini nyumba kubwa mara nyingi utapokelewa na neno "umechelewa wapi."?

3.Nyumba ndogo utapokelewa mizingo yako mlangoni na kwa mahaba huku ukivuliwa viatu lakini nyumba kubwa unaingia hakuna mwwnye time na wewe.

4.Nyumba ndogo ukifika unapashiwa chakula na maji ya kunawa mikono lakini nyumba kubwa ni kawaida kuambiwa chakula kipo hapo wakati huo mama wa nyumba kubwa kalala kwenye sofa anachati..

5 Nyumba ndogo unapewa maoenzi kama yote...mikunjo ya aina zote chumbani utapewa na maneno matamu ya mahaba lakini nyumba kubwa kifo cha mende pekee ndiyo kimebaki huku ukiambiwa "maliza haraka nataka kulala mimi "

6. Ukifika nyumba ndogo utakuta amevaa kimahaba..kila siku unavaliwa kimitego mitego lakini nyumba kubwa kitenge hicho hicho kila siku tena wengine cha sisiemu chenye picha ya JK kwa nyuma...

7.Ukitoka kwenye nyumba ndogo unasindikizwa moaka getini au kwenye gari lakini nyumba kubwa dada wa kazi ndiyo anaambiwa akakufungulie geti.

8.Numba ndogp sauti lainiiiii lakini nyumba kubwa maneno magumu kama kambi ya JKT..

9.Nyumba ndogo mtaoga pamoja kwa mahaba lakini nyunba kubwa kila mtu kivyake hata kama ni weekend wote mpo nyumbani..

10.Kwenye kulala nyumba ndogo anakukumbatia tightly lakini nyumba kubwa unapewa mgongo..

Haya ndiyo mambo machache yanayofanya nyumba ndogo izidi kushika kasi kila kukicha..

****wito wangu kwa nyumba ndogo, punguzeni mbwembwe mnafanya familia za watu wengine ziteseke sana...**

Post a Comment

0 Comments