NAMNA SAHIHI YA KUAMSHA HISIA ZA KIMAPENZI

Kawaida mahusiano ni kama kujenga nyumba ambayo ujenzi wake hudumu na kudumu hata kama ipo siku utaamua kuishi kwenye hiyo nyumba bado utaendelea na kufanya repair kila siku na kila mara.

Hivyo basi, ili ndoa yako iwe tamu na kuteka nafsi ya yule unampenda basi hakikisha huu mwezi unafanyia kazi mambo Yafuatayo;

Mapumziko ya pamoja
Inatakiwa kujadili na kupata muda wa kuwa peke yenu, hii inawezekana ikawa mara mbili au tatu kwa mwezi, hata kama mna watoto wengi kiasi gani lakini faraja inayotukuka katika mapenzi ni kuwa pamoja. Tafuteni siku maalum ambayo mtatulia, mtajadili mambo yenu kwa usiri na mtatenda chochote kinachostahili, hapa mtashangaa kuona mnatengeneza penzi ambalo kwa muda mrefu mlikuwa hamjalipata.

Watu wanaokaa pamoja wakajifungia sehemu kwa zaidi ya masaa matatu manne si rahisi kuwa na kisirani, kwa vile kwa kukaa hivi kila mtu anakuwa na muda mzuri wa kumrekebisha mwenzake.

Kutafuta raha katika mwili
Unatakiwa uwe mwepesi wa kuzigusa sehemu zinazomsisimua mwenzako hii inapendeza ikawa ni siku zile zile mnazoziteua kukaa pamoja, hata kama siku hiyo hamkuwa na ahadi za kutenda mambo yoyote ya kuchosha lakini ukishapita katika sehemu mbili kati ya 29 zenye raha basi ujue umetengeneza mapenzi mapya.

Kuondoa woga
Hili nimekuwa nikilipigia kelele siku nyingi kwamba mpenzi wako hustahili kumwogopa, japokuwa kuna mila kama hizo ambazo mumeo unaweza ukamuona kama baba, hii si mbaya lakini ubaba huu uwe na mipaka na inapofikia wakati raha inahitajika basi kila vurumai lazima zitumike.

Yapo mambo mengi sana ambayo unaweza kufanya ili kuhakikisha penzi na yule umpendaye linazidi kuwa na fukuto kubwa zaidi kama vile kupeana zawadi, kuhakikisha unaongea maneno yanayomtia moyo na kumsifia vitu anafanya nk.

Post a Comment

0 Comments