HUWEZI KUJUA MPAKA IKUKUTE, MSONGO WA MAWAZO NI HATARI ZAIDI

Jumamosi ya tarehe 31 Agosti 2019 baada ya kumshukuru Mwenyezi kwa kuniamsha salama salimini naingia mtandaoani kujua kilichojiri Duniani.Nikiwa na peruzi mtandaoni nakutana na habari ya kusikitisha kutoka huko Rombo Ambros Gervas Marandu (54) amekutwa amejiua kwa kujinyonga kwenye mwembe uliopo nje ya nyumba yake huku chanzo kikielezwa ni ndugu wa mke kukataa kumchangia pesa za kumzika mke wake matokeo yake marehemu hivyo kuamua kujitoa uhai.Kwa mujibu wa polisi Marehemu alikosa upendo na ushauri wa kimawazo.

Mbali na tukio hilo, mwezi huu pia tumesikia habari ya mwanafunzi mmoja kutoka Arusha Faisal Salum  akijua kwa kujipiga risasi huku taarifa zilizochapishwa na mtandao wa Mwananchi ukisema moja ya sababu ya kijana huyu kujiua ni kutokana na msongo wa mawazo ambao ulisababishwa na watu kusema kijana huyu anatumia madawa ya kulevya.

Habari kama hizi za watu kujitoa uhai wao zimekuwa nyingi sana kwa hivi karibuni. Watu wamekuwa wakichukua uamuzi huu wa kujiua baada ya kukosa usaidizi wa kimawazo.Kiukweli huwezi jua shida mtu anayoipata kama hujawahi kupatwa na tatizo hili. Mtu anaweza mlaumu mwenzie kwa maamuzi aliyoyachakua lakini nataka nikuambie hakuna tatizo linalosumbua kama hili la msongo wa mawazo. Ukiona mtu kachukua uhai wake au kafanya jambo flani usikimbilie kummbeza bali muombee huko aliko au msaidie kimawazo kwani neno lako linaweza kubadili mtizamo wa kile kinanchomsibu. Leo kwa kifupi nitagusia tatizo la msongo wa mawazo,chanzo,dalili madhara na jinsi ya kujisaidia au kumsaidia mwenye tatizo hili.


MAANA YA MSONGO WA MAWAZO

Mwandishi Sizarina Hamisi kutoka kenya katika Makala yake kuhusu msongo wa mawazo anasema ‘‘Msongo wa mawazo ni hali ya maumivu au mfadhaiko wa kihisia au kisaikolojia unaotokana na hali, tukio au jambo ambalo ni gumu sana au lenye changamoto kubwa.Tunasema una msongo wa mawazo pale ambapo unajisikia au unaona kama vile kila kitu kimekuwa kigumu.’’

CHANZO CHA MSONGO WA MAWAZO.

Ugumu wa kimaisha. Hii ni moja ya sababu kubwa inayopeleka mtu kuwa na msongo wa maisha.kundi kubwa linaangukia hapa.vijana wengi wanakumbwa na tatizo hili hasa waliomaliza elimu ya juu wakiamini wakitoka vyuo maisha yatakuwa rahisi lakini maombo huenda ndivyo sivyo.matokeo yake mtu anajikuta akiwa usiku kucha hasa akiona wenzako wametoa kimaisha yeye bado.

MAHUSIANO: Ukiachilia ugumu wa maisha , hii pia ni sababu nyingine imetajwa kusababisha watu kutumbukia katika msongo wa mawazo.sababu hizi ni kama kuachwa na mtu umpendae mathalani kuvunjika kwa ndoa, uhusiano wa Boyfriend na Girlfiend hupekelea mtu kuwaza sana matokeo yake anaangukia huku.

KIFO:hapa tunazungumzia kupoteza watu wetu wa karibu waliotangulia mbele ya haki. Wengine huwachukuwa mud asana kukubaliana na hali hii. Hivyo hupelekea kuwa na tatizo la msongo wa mawazo.

UGOMVI.Inaelezwa kuwa ugomvi pia usababisha mtu kuwa na msongo wa mawazo, Ugomvi huu unaweza kuwa ndugu kwa ndugu.

Sababu nyingine ni pamoja na maradhi ya muda mrefu, kufukuzwa kazini,kutamani vitu vikubwa hili hali huna uwezo.

DALILI ZAKE

Zipo dalili mbalimbali za kutambua tatizo hili na hapa ni baadhi ya dalili hizo.

Kukosa hamu ya kula

Kukosa hamu ya tendo la ndoa

Kukosa usingizi

Kuwa mtu wa hasira hasira

Kujitenga sana jamii

Mtu kujihisi mchovu kila wakati

MADHARA YATOKAYO NA TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO

Kujiua: Hii imekuwa kama njia ya watu wengi kujitibu tatizo hili.Tumeona hapo juu kuhusu matukio mawili kati ya mengi yanayosababishwa na watu kujitoa uhai kutokana na msongo wa mawazo. Madhara mengine ni pamoja.Kupungua kwa nguvu za kiume na za kike, Kupata tatizo la shikinizo la damu kutokana mtu kuwaza sana.

NINI KIFANYIKE UKIWA NA TATIZO HILI.

Mazoezi

Kuongea na watu. Wengi wanapenda kuweka vitu moyoni mwao ila inashauriwa kujitahidi kuongea na watu hata kama unahisi yule mtu hana uwezo wa kukusaidia kwani kitendo cha yeye kukubali kukusikiliza itakusaidia kwasababu mtu yule ameonesha upendo na kukujali.

Jikubali na kubali hali ilivyo sasa. Huwezi kuondoa tatizo kwa kuwaza sana.Mfano huna kazi,huna pesa ukikaa ndani ukiwaza maisha hayawezi kubadilika.Toka nje kapambani maisha mazuiri hayaji kama moto wa mshumaa unavyozimna ukipigwa na upepo hata giza linaingia usiku haliingii ghafla bali huja taratibu kuanzia machweo mpaka mawio ndipo giza uonekana.Hivi ndio ilivyo katika utafutaji wa maisha

Fanya ibaada. Ukiwa katika hali hii mrejee Muungu wako hakuna linaloshindikana kwake. Sikiliza visa vya mitume wake.Tazama kisa nabii Ayyub (JOB) katika Uislamu baada ya kupitia majaribu yote lakini hakumuacha Mungu. Tizama simulizi yake hapa

Post a Comment

0 Comments