HIVI KWANINI SINGLE MOTHERS HUWAGA WADHAIFU??

Kuna rafiki yangu mmoja hivi nilisoma naye chuo, huyu jamaa katika mwaka wake wa pili tangu aanze kazi alikutana na mfanyakazi mwenzie ambaye ni mtaalamu wa madawa ya binadamu (Pharmacist)

Wakaanza mahusiano ya mapenzi,lakini kiuhalisia jamaa yeye alikuwa naye kwa kujifurahisha tu kwa kuwa tayarialikuwa na mchumba wake lakini alikuwa anafanya kazi mkoa mwingine, akaamua amchukue huyu mfamasia kwa ajili ya kucheza rafu za hapa na pale na kuondoa upweke usio wa lazima.

Lakini kumbe mdada wa watu kajiongeza na hatimaye akamtegea jamaa siku zile za hatari, jamaa akiwa hana habari na mpango wa bibiye hatimaye akamtandika ujauzito, jamaa akaja juu kwamba kwanini ameshika ujauzito bila makubaliano? Akamwambia achoropoe,bibiye akagoma.

Basi jamaa kwa hasira akampiga kibuti demu,mahusiano yakafa lakini baadaye akasema wtashirikiana kumlea mtoto ila mapenzi yafe, mdada akasema haina shida.

Kwa hiyo kila mara wanatembeleana kwa ajili ya mtoto ila mambo ya mapenzi hakuna.

Sasa imepita miaka kama miwili hivi kajitokeza mshikaji mwingine anataka kuchukua mzigo jumla (kuoa), sasa katika process za utoaji barua, eti bibiye anampigia simu baba wa mtoto kuwa anataka kuolewa hivyo ampe ruhusa ya kuolewa ahahahahahhahahahah; jamaa akamwambia we olewa,unaniomba ruhusa kama nani wakati mi na wewe tulishaachana?

Kwa kufupisha stori, kiufupi pamoja na mchakato wa ndoa kuendelea lakini binti anaonesha matendo ya kidhaifu mno kwa mzazi mwenzie kiasi kwamba hata jamaa akiamua kuomba mzigo anaweza kupewa bila masharti; hali hii imefanya kutokea mgogoro mkubwa kati ya mume mtarajiwa na binti,mgogoro unaotokana na wivu wa mapenzi unaochagizwa na tabia ya binti kuwa dhaifu mno kwa mzazi mwenzie.

Kwa mujibu wa rafiki yangu anakiri kiukweli wakikutana na bibiye kwa ajili ya kumjulia hali mtoto, bibiye anakilegeza mno,yani anajiweka kiromantic na hayuko seriously sana kama mtu ambaye kweli anatarajiwa kuolewa.

Sasa, mimi naomba kuwauliza , Hivi ni sababu ipi haswa inayopelekea mabinti wengi kuwa dhaifu kwa wanaume waliozaa nao kiasi cha kuwapa wakati mgumu waoaji?

Hivi haiwezekani mkizaa mkaachana moja kwa moja bila kuwa na shauku ya kukumbushia mapenzi?

Post a Comment

0 Comments