DALILI ZINAZOONYESHA MWANAMKE ULIYENAE ATAKUSAIDIA KULETA MAFANIKIO

Katika moja ya Interview ambayo Barack Obama alifanya na jarida la “Black Enterprise Magazine” la nchini Marekani, muandishi alimuuliza kuhusiana na hali ya uchumi ya Marekani.

Aliulizwa, “Bwana Obama, Je una hofu juu ya hali ya uchumi wa Marekani inavyoenda?”
Ambapo Obama alijibu, “Hapana, sihofii uchumi wa Marekani, nina hofu na mke wangu..kwa sababu ana idea nyingi kichwani mwake mpaka nashangaa”

Hivyo, kama unae mwanamke anaekutia moyo ufanye vizuri zaidi. Huyo mwanamke ni keeper, kama hujamuoa, basi anastahili pete kidoleni kwake.

Hapa chini nimeelezea njia  zitakazokuonesha kwamba Girlfriend wako anafaa kuwa mke kukusaidia ndoto za mafanikio na ndoa imara!

1. Anavaa kimafanikio (she dresses for Success, not to Seduce)
Kama kitu ambacho kinawatofautisha wanawake wenye mafanikio na wengine ni mavazi wanayovaa. Wanawake wasio na focus huvaa mavazi ya kushawishi, lakini wanawake walio focused huvaa nguo za heshima. Wanawake wote wenye mafanikio kwa jitihada zao halali huvaa kiheshima, kuanzia Marissa Mayer, Oprah Winfrey au Michelle Obama. Kile unachovaa, kinaeleza kwa undani namna tabia na mwenendo wako ulivyo.

2. Huishi kulingana na kipato alichonacho.
Hii haimaanishi anaishi kimasikini. Hapana, inamaanisha anampangilio mzuri wa fedha anazozipata kwa halali yake. Kwamba katika fedha yake, anayapa kipaumbele mambo ya msingi, kwamba yuko tayari aishi kwa kujibana sasa hivi ili baadae aishi kama Malkia.

3. Hana marafiki wengi na amezungukwa na marafiki ambao ni problem solvers na sio attention seekers.
Hebu nioneshe mwanamke yeyote mwenye mafanikio, na mimi nitakuonesha mwanamke mwenye mtandao wa marafiki ambao ni World changers wale wanawake wanaopenda mafanikio.

Kama Zig Ziglar alivyowahi kusema kwenye kitabu chake cha “Over the Top”, “Zungukwa na watu ambao watakutia moyo na watakupa hasira ya kuinuka juu ya pale ulipo”
Hivyo, utatambua mwanamke wako atakuja kuwa vipi kwa kuangalia marafiki anaochangamana nao.

4. Huilaumu nafsi yake, sio jinsia yake.
Tofauti na wanawake wengine, mwanamke mwenye kiu ya mafanikio hapotezi muda kulalamika kuhusu vikwazo anavyopata kwenye biashara au kazini kutokana na jinsia yake pale anapofeli jambo. Badala yake, hukabiliana na changamoto za yeye kuwa mwanamke kazini, na kuzitafutia ufumbuzi. Hautakuja kusikia mwanamke mwenye mafanikio analalamika kufeli jambo kisa yeye ni mwanamke.

5. Huwa na imani ya mafanikio.
Namaanisha, hujiamini na huiamini nafsi yake kuwa anao uwezo wa kufanikiwa. Kama founder wa magari aina ya Ford Ranger, Henry Ford katika kitabu chake cha “My life and Work” alivyosema kuwa, “Uko sahihi vyovyote vile utakavyofikiria, kama utafikiria unaweza uko sahihi, na kama utafikiria hauwezi uko sahihi vilevile”

6. Huwasaidia wanawake wenzake.
Moja ya jambo ambalo nimejifunza katika maisha yangu ni kwamba, tofauti na wanaume ambao ni rahisi mno kuinuana na kusaidiana kwenye matatizo, wanawake hawapendani, na baadhi hufurahi wanapoona wenzao hawafanikiwi kuzidi wao.

Mwanamke wa kwanza kabisa kuwa secretary state wa Marekani Madeleine Albright amewahi kusema, “Kuna sehemu yao mbaya sana kwa wale wanawake ambao hawataki kusaidia, hawawapendi na wana wivu juu ya wanawake wenzao”
Mwanamke wako atafanikiwa, endapo atawapenda wanawake wenzake na kuwasaidia na wao wafanikiwe.

7. Yupo current, yuko updated na anafahamu mambo mbalimbali yanavyoenda.
Hii inamaanisha anajitahidi kuji-expose na maarifa mapya, taarifa, na idea mbalimbali ambazo zitamuinua kiakili na kifikra. Funguo za mafanikio zipo katika maarifa mapya. Kama Brian Tracy alivyowahi kusema, “to earn more, one has to learn more”

8. Yuko radhi kubeba risks.
Hii inamaanisha haoni hasara kupoteza katika uwekezaji, sio kwenye biashara tu, hata kuwekeza moyo wake kwako. Hata kama ataona haufanikiwi kwa hivi sasa, atakuamini, kiasi ya kwamba atawekeza roho yake, akili yake na hisia zake kwako.

Ngoja nimalizie kwa Hekima hii, Uwekezaji ulio bora kwa mwanamke sio kujaza nguo kwenye kabati, uwekezaji mzuri ni kupata yule mwanaume bora ambae MUNGU amekuchagulia!!

Post a Comment

0 Comments