CHANZO CHA MAHUSIANO KUKOSA MVUTO

Wakati tunaingia kwenye mahusiano tunahurusu sana moyo kuchukua nafasi kubwa kuliko akili zetu,matokeo yake ni pale unaeza kuta watu wanadiriki hata kusema kuwa mtu kalishwa limbwata,ila ukweli ni kwamba mtu huyo anatumia moyo sana badala ya akili...

Ukweli unaoumiza ni kwamba wengi wetu tupo kwenye mahusiano na hatukuzingatia vitu vya msingi,tulijitoa akili....umewahi kujiuliza kwa mwenzi wako ukiachana na uzuri,mapenzi na making of a family anaweza kuwa na msaada gani mwingine!?....

Changamoto inakuja baadae unakuta vitu ulivyompendea vyote vishakuwa vya kawaida,huyu mpenzi wako thamani yake inaisha,na kwa taarifa yako vitu ambavyo haviwezi kuzuga hata kidogo ni Moyo,lazima utabadirika tu na mabadiriko yataonekana wazi,utaanza complaints hata kwa vitu vidogo ambavyo mwanzo pengine ndio ilikuwa kiashirio cha mapenzi...mf.kupiga simu mara kwa mara,kulalamika kuchelewa kurudi,kuona marafiki ni bora nk.

Sasa kila kitu kinahitaji suluhisho au mawazo ya kujenga,leo wananzengo tujadiriane tunachojua kuhusiana na mahusiano kuanza na kuisha kwake,wewe unajua unachokijua na mimi najya ninachokijua,tusaidiane kimawazo wapo wanaoumia na wanashindwa kusema....hata mwenyewe naumia hapa,sielewi ilikuwaje hadi saiv kitanda cha tano kwa sita nalala peke angu,wakati ilikuwa tunalala watatu yaani mimi mama maria na maria wakati akiwa mdogo...

Post a Comment

0 Comments