Mwanamke mmoja nchini Marekani amefanyiwa upasuaji baada ya kyivuta peke yake ya ndoa kutoka kwenye kidole chake na kuimeza wakati alipokuwa amelala fofofo
Jenna Evans, mwenye umri wa miaka 29, amesema kuwa mchumba wake Bobby alikuwa katika treni ya mwendo kasi na akalazimika kumeza pete ili kuilinda dhidi ya "watu wabaya".
Alipoamka katika nyumba yake mjini California aligundua kuwa alichofikiria kilikuwa ni ndoto tu , lakini akagundua kuwa pete yake haipo kidoleni.
Alisema kuwa alipogundua hilo , alimuamsha Bobby kumuelezea, na ndipo wapenzi hao wakaenda hospitalini.
Bi Evans anasema alihangaika kukumbuka kisa hicho ili kuwaeleza madaktari ''kwasababu nilikuwa ninacheka na kulia sana ".
Picha za skani ya X-ray zilibaini kuwa pete hiyo ilikuwa ndani ya tumbo lake, na madaktari wakakubaliana kuwa lingekuwa si jambo la busara ''kuiacha ijiondoe tumboni yenyewe kwa njia ya choo''
Bi Evans, ambaye ni mkazi wa San Diego , baadae alifanyiwa upasuaji wa kuiondoa pete hiyo lakini alitakiwa kusaini fomu za kukubali kufanyiwa upasuaji huo, ikiwa kifo kingetokea.
"Halafu nikalia sana kwasababu ningekuwa mjinga sana kama ningekufa ," alisema. "Niliisubiri sana pete hii ya uchumba na nitaolewa na Bobby Howell."
Upasuaji ulikuwa wa mafanikio , na Bi Evans anasema baada ya kugutuka bada ya upasuaji alianza " kulia sana".
"Nilifurahi sana kwasababu siwezi tena kuiangalia na kuithamini kama ilivyokuwa awali ," alikiambia kituo cha televisheni cha ABC news.
0 Comments