ZIJUE SIFA ANAZOANGALIA MWANAUME KABLA YA KUOA

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote jambo kwanza huchekecha akili.

Hutumia muda mrefu kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapendwa ni uzuri na kujikuta akipoteza muda wake mwingi kutaka kuonekana ana mvuto ili kumpagawisha mwanaume uliyenaye.

Kuna vitu ambavyo wanawake wenzangu mnajisahu kinachoangaliwa katika kuolewa si uzuri tu yapo mambo muhimu yanayoangaliwa zaidi ya hayo ya uzuri wako.

Unaweza ukawa ni mzuri lakini tabia zako ni mbaya mwanaume anafikiria kukuweka ndani itakuwa pasua kichwa na kuamua kuwa na wewe kwa ajili ya kukutembezea mashine lakini hana malengo ya kukuoa.

Jambo ambalo mwanaume huangalia anapotaka kuoa kwanza huangalia mwanamke mwenye mapenzi ya kweli.

Hapa naomba tuwekana sawa wanawake wenzangu wapo baadhi ya wanawake hawana mapenzi ya kweli wanaangalia mwanaume mwenye fedha zaidi alafu anategemea kuolewa.

Kwanini wanaume wanapenda mwanamke wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu chenye raha tu.

Kuna wanawake wengine wao wanataka maisha ya raha ikitokea shida hawataki kuelewa na ndoa kuikimbia.

Jambo jingine tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.

Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia ama wengine kuangalia shepu matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

Pia wanaume huangalia mwanamke mwenye uchu wa maendeleo hawapendi kuoa mwanamke ambaye hatakuwa na kazi basi kama hana kazi awe na uchu wa maendeleo ama kujikita katika biashara ama kilimo.

Jambo jingine ambalo wanaangalia ni uaminifu wako. Mwanamke unatakiwa kuonyesha uaminifu kwa mwanaume wako acha kufanya mambo kiusanii. Hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo wanaume wanaangalia.

Kuna baadhi ya wanawake wanaona ukimkatikia mwanaume hapo ndio utaipata ndoa unaweza kukatika hadi nyonga ikapinda na ndoa ikaenda kwa mwingine.

Hivi unajisifu unajua kukatika alafu hauna maadili ya kumfanya mwanaume akuoe kweli?? Mbona ndoa utaisubiri sana.

Wanaune hawaangalie kukatika kwako je una maadili ambayo yanamfanya akuweke ndani??
Jitafakari na kuchukua hatua.

Post a Comment

0 Comments