YAJUE MAMBO YANAYOMPA FURAHA MPENZI WAKO


Uhusiano maridhawa katika ndoa ni kitu kinachohitaji kujituma kwa bidii kubwa. Ni kitu kinachohitaji subira, uelewa na upendo kwa pande zote mbili.

Wakati unapenda kumfanya mwenzio kuwa mwenye furaha, kuna mambo kadhaa unayoweza kuyafanya kuhakikisha nawe unapata furaha. Ukweli kama hutofanya mambo haya matano, hutokuwa na zana sahihi zinazokupa furaha katika maisha ya ndoa yako:

1. Kumuamini.
Imani ni ufunguo wa furaha katika maisha ya ndoa. Usipomuamini mwenza wako utaendelea kukosa utulivu na kuwaza kuwa yuko wapi, yuko na nani au anafanya nini. Stress na mashaka utakayoyapata kutokana na wasiwasi na hisia za kuhisi kile anachofanya vitakuondolea furaha  yako.

Ili uwe na furaha unatakiwa kuwa na imani, kumuamini. Imani inaweza kuchukua muda mrefu kuijenga, lakini ni kitu nyeti sana. Hakikisha unamweleza mwenzako wasiwasi wako pindi jambo fulani linapokuwa haliko sawa. Inaweza ikawa ni kutoelewa tu, lakini ukiiruhusu shaka ishike hatamu, inaweza kugeuka kuwa tatizo kubwa zaidi. Usiiruhusu shaka itawale maisha yako. Usiiruhusu shaka ndio iongoze maisha yako. Jiamini na umuamini, hiyo ni dawa kiboko.

2. Kumpa nafasi.
Kama unataka kuwa na furaha na mumeo hakikisha unampa nafasi, usimbane. Muache ajumuike na marafiki zake au kushiriki mambo ya maana anayoyapenda. Humfanya apate fursa ya kuwa mbali nawe kwa muda fulani na kuongeza nishati mpya ndani ya moyo na akili yake.

Sio tu kwamba ataku-miss, bali pia itakupa fursa ya kuwa mbali naye. Mkitumia muda wote wa 24/7 kuwa pamoja haliwezi kuwa jambo zuri, na halitokuwa na afya kwenye uhusiano wa ndoa yenu. Anaweza kuwa na hisia za kudumaa au kuhisi kuwa hawezi kufanya vitu anavyopenda kuvifanya. Mnapopata fursa ya kuwa mbalimbali kwa saa kadhaa inawapa fursa ya kuungana tena baadae mkiwa na nguvu mpya.

3. Kutenga muda wa kukaa pamoja.
Wakati fulani tunashughulishwa mno na shughuli za maisha na utafutaji kiasi kwamba hatutengi muda kwa ajili ya wenza wetu. Ili kuwa na furaha ni muhimu kutenga muda maalum kwa ajili yake tu, hata kama ni dakika chache. Pia wekeni muda maalum kila wiki kwa ajili ya kunong'onezana ambapo hakuna watoto, hakuna marafiki au kitu kingine chochote, ni nyinyi wawili tu. Kumbushieni mahabba yenu na ladha ya muunganiko wenu.

Pia ni jambo zuri kutenga dakika kadhaa kila siku kwa ajili ya kuwasiliana. Mnaweza kutumia muda huo kujadili siku yenu inavyoendelea au kuchombezana. Kuwa na utaratibu wa kutenga muda maalum wa kuwasiliana au kuwa  pamoja utaupa nguvu uhusiano wenu na kukufanya kuwa mwenye furaha.

Post a Comment

0 Comments