Ni asubhi, naamka nawahi kituo cha mabasi madog almaarufu daladala, nasubiri zile ziendazo Igoma na zitokazo buhongwa (jijini Mwanza), napanda safari inaanza, huku dereva akipiga ule wimbo walioimba vijana wa TMK Temba na Chege, ‘VIJANA FUNGENI MKANDA’
Tunafika kituo cha sahara (City center) nasikia kelele zilizo ashiria kuna malumbano, inanifanya nichungukie dirishani, naona ni watu walio katika rika tofauti,’WAZEE DHIDI YA VIJANA’ inanivutia zaidi na kusikiliza kwa umakini ili nijue ni kipi hasa kinachowafanya asubuhi ile kupigizana kelele.
Mara nasikia mzee mmoja akisema” vijana wa kileo ni wavivu wa kila kitu, kuanzia fikiri mpaka kazi, hawana cha maana zaidi ya kupendeza na mapenzi”, Papo mzee mwingine nae anakazia kuwa ” ujana ni ujasiri, ubunifu, na utenda kazi, enzi zetu karne ya 20 hatukuwa tumelemaa namna hii, tulimaliza shule na vyuo na kujiajiri, wala hatukusubiri serikali itupe ajira kitu ambacho ni tofauti na vijana wa kisasa wa karne 21″. nikibaki nikijiuliza huku kondakita akipiga debe gari lijae tuendelee na safari ya Igoma, najiuliza nini chanzo cha mjadala huo, mara kijana moja aliyekuwa amaeshika bahasha na muonekano wake wa kitanashati anasema kuwa ” nyie vizazi vya karne 20 acheni majivuno, kwani enzi zenu hapakuwa na changamoto kama za wakati huu, moja mlikwa wachache na mambo yalikuwa mengi, kwa sasa vitu vingi vimebadirika”,.
Nikizidi kupata picha ya ya kile walichokuwa wakilumbana, mzee moja aliyekuwa amevalia kibaraghashia anaibuka na kusema ” hamna hoja kijana, kutwa mitandaoni, elimu mlionayo siku hizi ni makaratasi tu! ni elimu tegemezi, haimwandai kijana kujitegemea, na ndo chanzo cha vijana wengi kulia hakuna ajira, kikuu ni elimu na uzembe wa vijana”. nashangaa kwa nguvu! inabidi nishuke pale pale nighairishe safari ya Igoma, ili niwepo kwa ukaribu nisikilize vizuri hoja zile.
Baada ya kama robo saa hivi, nikisikiliza malumbano yale, naamua kwenda kioski kilichokuwepo jirani kidogo! nachukua ‘APPLE PUNCH’ baridiii kabla ya chai.
Naangalia pembeni kuna kijiwe cha fundi viatu, nafuta benchi nakaa nikinywa huku kubwa zaidi nikitathimini na kuwazua juu ya ile mada iliyokuwa ikiendelea pale stendi ya Sahara mjini, huku nikikumbuka ule wimbo wa Mwanazuoni aliyekomaa na msanii wa kizazi kipya wa kipindi kile SOLO THANG wimbo wake ule “HOMA YA DUNIA”.
Ubaridi wa ‘Apple punch’ unanipa picha ya mada nzima ni kwamba!.
“ WAZEE WANASEMA UDUNI WA ELIMU WAIPATAYO, UZEMBE NI CHAZO CHA VIJANA WENGI TANZANIA KULIA JUU YA AJIRA” (Unemployment)
JE,NIKWELI? Vijana wa karne 21, ni wazembe? wavivu wa kufikiri? JE elimu ya Tanzania ya karne hii 21 ni butu? tegemezi? ni duni? ikilinganishwa na ile ya karne 20? vyuo vikuu hivi kwa sasa elimu yao ni duni? ikilinganishwa na ya enzi za mwalimu? .HOPO TWENDE SAWA!
HOJA YANGU NI KWAMBA!
Huku dunia na nchi zilizoendelea nazo zikiangaika kutibu homa hii ya dunia (unemployment) wakikiri kuwa teknolojia ndo mchawi mkuu aliyoroga dunia, sisi Tanzania bado tukiamini kuwa uzembe wa vijana na elimu ya 21 ndo vyanzo vikuu kwa hili.
Ndio sipingani juu ya madai hayo, kuwa elimu yaweza kuwa nyemelezi juu ya homa hii,lakini sio kirusi cha homa hii, kwa maana kwamba! kirusi kikuu ni mapinduzi ya teknolojia. Si kwamba elimu ya karne ya 21 ni duni la hasha, bali kwa mantiki ya uhai wa elimu, ya kuwa, elimu ni kama shilingi inapande mbili, ya kuwa na ‘ theory’ ambapo tunaangalia ubora na upande wa pili ‘ practical’ ambapo tunaangalia uhai wa elimu husika, kwa upande wa ubora elimu yetu Tanzania bado ni bora sana, lakini kwa upande wa uhai amabapo imeegamia katika maswala ya sayansi, na sayansi tunazungumzia teknolojia bado tupo chini kwa kiasi.
hivyo! si vyema kuzungumzia ubora bali tuzungumzie uhai wa elimu katika swala la ajira, hapo pia tunazungumzia teknolojia katika mawanda ya elimu..
Je uhai wa elimu yetu inaathari gani katika soko la ajira kwa vijana wengi?
Athari ipo, pale kijana anaposoma masomo bila kufanya vitendo, hasa masomo ya sayansi ambapo inaweza kuathiri hasi ufanisi wake katika kufanya kazi ya kile alichosomea, lakini bado sio kwa kiasi kikubwa kuwa elimu yetu sio hai,Ndo sababu watu hawapati ajira, kwa sababu tunaona vipo vyuo vingi vya ufundi na utabibu vina vitendea kazi vya kisasa na wanafunzi wanamaliza masomo yao wakiwa na uweledi wa hali ya juu na bado hawana kazi ya kufanya, wapo mitaani.
Mi naona athari kuu sio elimu kwa sababu hata nchi zilizoendelea mfano Canada, marekani, uingereza,uchina napo bado tatizo la ajira lipo kwa kiwango kikubwa tu, japo sio kama afrika,
Hivyo! nahisi mapinduzi ya teknolojia na kutumika katika maeneo ya uzalishaji na uuzaji yaweza kuwa sababu kuu, mfano leo hii zipo mashine viwandani ambazo zinafanya kazi ambayo ilikuwa ifanywe na zaidi ya watu 50 kwa siku, zipo kompyuta ambazo kimsingi zimechukua ajira za watu, lakini
Sio katika maeneo ya kazi tu! teknolojia imeathiri mtindo wa vijana wengi duniani hasa afrika hasa pale jamii zetu zinapopokea huduma au bidhaa hizi za kiteknolojia na kupelekea kulemaza fikra za vijana wengi katika suala la utafutaji na fikra, mfano mdogo tu afrika yetu!
*mchezo wa pool table
*mitandao ya kijamii
*simu janja n.K.
KATIKA FIKRA KWA VIJANA.
Si kwamba vijana wa karne 21 hawana fikra nzuri au wazembe hapana! wapo lakini lazima tukubari teknolojia imechochea mabadiriko ya mitindo ya maisha kwa vijana wengi, kitu ambacho kimeathiri sana maisha ya vijana wengi ukilinganisha na vijana kutoka nchi za magharibi,
Katika nchi zilizoendelea michezo kama pool table, meza za kubeti, kamali nk. Huchezwa na watu wenye umri 18+ na kuna mahali mahalumu ambapo vinapatikana mfano katika kumbi za starehe ambapo sheria husimamaiwa kikamirifu kutoruhusu mtoto kushikiriki, kutokana na athari kubwa itokanayo na michezo hiyo, kitu ambacho tofauti na Afrika ambao michezo hiyo inachezwa kila mahali na imewekwa kama chanzo cha mapato kwa mtu hadi taifa kwa ujumla bila kujari ni athari zitokanazo na michezo hiyo katika jamii husika, hivyo hivi vyote ni teknolojia inatumika kuua fikra za vijana wa kiafrika.
Vipo vingi kama umiriki wa simu njanja, mitandao ya kijamii, matumizi ya wanajamii wa kiafrika yapo tofauti sana na watu wa magharibi, vitu hivi vina haribu sana na kulemaza fikra za vijana kisaikolojia. Ni ulevi wa akiri usiotokana na pombe.
Hivyo sioni sababu ya wazee kubeza elimu ya karne 21, kwani elimu hii bora zaidi kuliko ile ya 20 karne, huwezi kusema UDSM ya 1980’s ni bora kuliko ya 2001’s kimiundo mbinu, wakufunzi, nk. Huwezi kusema SUA ya 1980’s ni bora kuliko 2001’s hapana, bali ni mtindo wa maisha ya jamii ya sasa.
Si kwamba! vijana hawapendi kujiajiri, lakini mazingira hayo yapo? je vip kuhusu mikopo kwa vijana wamalizapo vyuo na vyuo vikuu?
Je ni sahihi kumpatia mtu mkopo wa kusoma alafu akishamaliza chuo akae tu, au ni sahihi pia kuwepo na taasisi ya serikali ambayo itatoa mikopo kwa vijana hata pindi wamalizapo vyuo ili waweze kujiajiri? nk. Alafu wanarudisha mkopo wa elimu na mkopo wa fursa kwa pamoja, nahisi inge kaa vyema sana, sio kusema vijana wanawaza kuajiriwa bila kuwaandalia mazingira ya kuwaza kujiajiri.
Zipo sababu zinazopelekea vijana kulia ajira, mfano! UMASIKINI ni sabau kuu, umasikini kwa kijana husika, mtu kamaliza pale DIT na anaujuzi mzuri tu, lakini hana pesa ya kuazisha kalakana yake ya kutengeneza magari sababu ya umasikini inambidi atafute kazi ili apate, lakini umasikini wa Taifa, nchi za afrika hazina pesa ya kuwalipa vijana ujira.
Mfano tu, katika sekta ya afya, elimu, polisi, sheria, uandisi, sekta hizi ni nyeti na zinaitaji watumishi wengi sana hasa afrika, lakini ni madaktari wangapi mpak leo hawana ajira? wauguzi, waandisi, walimu, wanasheria, si kwamba serikari haioni huitaji wa kuwa na watu hao lakini ni umasikini wa kuwalipa mishahara watu hao, unakuta shule hakuna walimu, vijiji havina polisi, hakuna madaktari wa kutosha, na watu wapo wamesoma na wamefaulu vizur lakin serikal haina fedha ya kuaanjir watu wote.
Lakini vile vile, ongezeko la watu, nayo yaweza kuwa sababu ya ajira kuwa ngumu kwa vijana.
Sioni haja ya kutoa lawama kuwa vijana wa sasa kuwa ni wavivu na elimu yao ni duni, hapana, inabidi tuangalie kwa jicho la tati nini chanzo cha yote haya? kuanzia katika jamii tunazoishi,
Mwisho ni kwamba!
( Tatizo linalosababishwa kiteknolojia, litatatuliwa kiteknolojia na si vinginevyo, kisiasa nk. Hivyo vijana, wazazi, serikali na jamii kwa ujumla iamini katika teknolojia na iwekeze ili kutibu HOMA HII, bila kusahau sheria na kanuni kwenda na wakati pindi teknolojia inapobadirika ni vyema kubadirika pamoja ili ije na sheria na kanuni ili kulinda vizazi husika.)
SHABAN SADICK MWANDISHI WA MAUDHUI YA MTANDAO. UNAWEZA NIFUATA INSTA KWA JINA LA LAKITANZANIA.
0 Comments