NJIA ZA KUEPUKA HASIRA.
1⃣: Epuka Mabishano:
✍🏼Mara nyingi hasira hupandishwa na mabishano baina ya mtu na mtu/watu. Njia kubwa na rahisi ya kuepuka kupandwa na hasira, ni kwa kuepuka kubishana na mtu au watu, hasa wale wanao onekana wagumu kuelewa. Penda kuepuka kujibizana au kumjibu mtu kwa ukali.
2⃣: Penda kujishusha:
✍🏼Unapogundua umemkwaza mwenzako, na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu na yenye ukali, basi penda kujishusha na kuzungumza kwa utaratibu, au kuomba radhi. Hii husaidia kumshusha hasira mwenzio, kushuka kwa hasira kwa mwenzio husaidia kushusha yako pia.
3⃣: Jifunze kuwa na matumizi mazuri ya kinywa:
✍🏼Mara nyingi kinachompandisha mtu hasira huwa ni kauli chafu. Jifunze kuwa na kauli njema itakusaidia kuepuka migogoro ambayo itakufanya upandwe na hasira au umpandishe mwenzio hasira. Hasa kauli zenye kujaa matusi, kejeli, au dharau hupandisha mtu hasira. Na sauti yenye ukali, kukoroma, au ukaripiaji, humpandisha mtu hasira.
4⃣: Penda kudharau watu:
✍🏼Dharau tunayo izungumzia hapa sio ile dharau ya kumbinulia mtu mdomo, wala kumshusha na kumpandisha macho. Hapana, kudharau means “Humpi mtu attention anayoitaka ili kugombana na wewe ” Ukiona mtu anakutusi, analeta kejeli, au hata kuleta shari. Njia pekee ya kumuepuka ni kwa kumdharau kama mtu asiye na akili, aliyekosa heshima na maadili. Hivyo hujibizani nae, wala kumpa attention anayoitaka.
5⃣: Penda kuheshimu upeo wa mtu:
✍🏼Binadamu tumetofautiana upeo wetu wa kutafakari, kuelewa, na kujibu jambo, hivyo sio kila wakati mtu atakujibu au kufikiria kama ulivyotaka akuelewe. Ukiona umemuambia mtu kitu halafu akakujibu hovyo, basi chukulia kama ndipo uwezo wake kufikiri ulipoishia. Kama unaweza kumrekebisha basi tumia lugha safi, na sauti iliyojaa upole, na umueleweshe kwa hoja zilizo jaa hekima na busara. Kumjibu hovyo pia huweza kuleta mtafaruku kati yenu.
6⃣: Jifunze kuishi na watu:
✍🏼Binadamu tumetofautiana historia zetu, kuendana na jamii tulizo ishi na aina ya maisha tunayopitia. Kuna watu wakali, kupenda ugomvi, hasira za karibu, gubu/ulalamishi, ndio tabia zao. Hata ukizungumza jambo la kawaida huwa wanalikuza. Hivyo ni vyema kujifunza kuishi na watu wa aina hii, na njia pekee ni kuepuka kujibizana nao.
7⃣: Penda kusoma mood ya mtu:
✍🏼Ukiona mwenzio kapandwa na hasira, usijibizane nae. Ukiona yuko na uchovu, usipende kumsumbua wala kumlalamikia jambo. Ukiona yuko na stress, mpe tulizo, usimsumbue wala kumkaripia. Ukiona yuko na hofu kupindukia, usimtishe kwa lengo la kumcheka, mpe tulizo. Ukiona ana huzuni aidha amefeli jambo, au amefungwa team yake, au ameondokewa na kitu, au kakikosa, basi ni vyema kumfariji badala ya kumtamkia maneno ya kukera, kuudhi, dharau, au kejeli. Hii itakusaidia kuepuka kugombana nae.
8⃣: Penda kuelimisha:
✍🏼Wengi wetu tunapenda kuwa walalamikaji, ukaripiaji, na ndio tunachukulia kama njia sahihi za kutoa madukuduku yetu. Tunakosea sana, hapo lazima utamkera mtu. Njia nzuri ni kujifunza kumuelimisha mwenzio pale anapokosea, kumshauri, na yote yatumie sauti tulivu na kauli nzuri. Hii itasaidia kuepuka ugomvi, achana na tabia ya kumtukana, kumlaumu, kumkaripia mwenzio. Hii itampandisha hasira, na itakupandisha hasira wewe pia pindi ukijibiwa hovyo.
Hizo ni njia za kuepuka wewe kupata hasira, pamoja na kuepuka kumpandisha hasira mwenzio.
NJIA ZA KUTIBU HASIRA YAKO.
✍🏼Ukiona ushaanza kupandwa na hasira ni vyema kukaa kimya, epuka kujibizana na mtu ili kuepuka ugomvi, au kuepuka asikujibu mambo yatakayo kupandisha hasira zaidi. Au kama unaweza basi badilisha mada, au kama haiwezekani, endelea kunyamaza ili kuepusha shari.
✍🏼Jifunze jinsi ya kukaa na mtu mwenye gubu, lawama, ukiona kashaanza lawama tu basi shusha sauti yako haraka sana, au nyamaza, au omba udhuru utoke mara moja.
✍🏼Mtu anapokuudhi jifunze kubeba maumivu, vumilia na ujishushe sababu kuendelea kujibu kwa ukali hukufanya uzidi kupandisha hasira. Hii itakusaidia kipindi uko kwenye sehemu ambayo huwezi kuondoka karibu na aliyekuudhi…mfano: Kwenye (matatu) daladala.
✍🏼Ukiona ushaanza kukasirika basi ondoka mahali penye mabishano.
✍🏼Ukipandwa na hasira, epuka kukaa karibu na aliyekuudhi, au kukaa karibu na silaha yeyote.
✍🏼Pata glass moja ya maji pindi unapoona hasira zimekupanda.
✍🏼Ukijijua una hasira kali zinazoweza leta madhara, ni vyema ukajizuia kufanya maamuzi yoyote. Na njia sahihi ni wewe kukaa mbali na eneo la tukio.
✍🏼Kusali/kuswali husaidia kushusha hasira.
✍🏼Kuna nyakati inakuwa ngumu kuzizuia hasira sababu uko katika mazingira ambayo huwezi kuondoka, na huwezi kuvaa earphone ili usimsikilize sababu ni mtu unaye muheshimu. Hapa ndipo unapotakiwa kujifunza kuwa kuidhibiti hasira huanzia ndani ya nafsi yako mwenyewe. Nyamaza kimya, msikilize yeye. Anza kujenga mawazo ya kitu kingine tofauti “Mfano: Dah lile pilau la jana”. Hii itakusaidia kuufanya ubongo wako usitafsiri zile kelele zake zinazopita masikioni mwako. Na kuufanya ubongo uwe na mawazo tofauti kabisa.
✍🏼Unadhani hii inafanyaje kazi??? Hebu fikiria, ulishawahi kuwa darasani, mwalimu anafundisha, lakini mawazo yako mbaali.
✍🏼Mwisho unashtukia kipindi kimeisha na hujui kilichofundishwa.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.
✍🏼Epuka kubaki na kinyongo au chuki kati yenu, jifunze kusamehe pale hasira zinapoisha. Na kama ni mtu wa karibu, basi ni vyema mkaya suluhisha au kusameheana bila kuombana msamaha. Chuki huzalisha madhara mengi zaidi.
✍🏼Epuka kununa nuna baada ya hasira kuisha, hii itakusaidia kukuacha huru bila stress za mtu yeyote. Onyesha tabasamu pale hasira zinapoisha.
✍🏼NB: Wanaume ni vyema kujifunza kuwa mpenzi wako akikununia baada ya kukorofishana, haimaanishi kuwa ndo hataki kuwa na wewe tena. Wengine hununa kwa nia ya kutaka kubembelezwa, anahitaji kuiona thamani yake kwako.
✍🏼Hata hivyo, hizi ni njia ambazo wewe utazitumia kuendana na eneo ulilopo, na ukubwa wa tukio. Mara nyingi ukifatilia wanaopandwa na hasira huwa inatokana na wao kupenda kujibizana na mtu, tena kwa maneno ya kukera, na sauti ya juu. Hapa lazima utapandwa tu na hasira, na mwenzio atapandwa na hasira.
Mwisho mnapigana.
.
✍🏼Ukitazama sana watu wanaoudhi wenzao, utagundua ni kwasababu hawajui kusoma mood za wenzao, hawajui kutumia vinywa vyao vizuri ili kuwasilisha jambo. Wanapenda kulalamika sana na kutumia kauli chafu na sauti kali.
.
Mungu awabariki sana na kuwafanyia wepesi.
Jifunze kuwa kimya HASIRA inatibika
0 Comments