WANAFUNZI WAINGILIANA KINYUME NA MAUMBILE KUKWEPA UJAUZITO

Baadhi ya wanafunzi wa kike katika Shule za Msingi na Sekondari jijini Mwanza, wamedaiwa kujihusisha na mapenzi ya kinyume na maumbile, kwa kile kilichoelezwa kukwepa kubeba mimba na kupelekea kufukuzwa shule.

Hayo yamebainika mkoani Mwanza kwenye kikao cha wadau wa elimu, kilicholenga kujadili mkakati wa kutokomeza mimba za utotoni ikiwemo kutoa elimu juu ya madhara ya kufanya mapenzi, katika umri mdogo.

Matoke Jackson ni Mkurugezi wa Asasi ya Usaidizi wa Kisheria ya Wilaya ya Ilemela (ILABU) ameibainisha kuwepo kwa tatizo hilo kwa changamoto hiyo kwa wanafunzi hasa wa shule za msingi kujihusisha na mapenzi ya kinyume na maumbile.

“Kwenye utoaji wa elimu hii tumegundua mpaka Shule za Msingi sasa ni tatizo, mpaka watoto wa Darasa la nne wanajua namna ya kufanya mapenzi, tena hasa ya mapenzi ya kinyume na maumbile, yamelipuka sana kwenye Shule za Msingi kuliko za Sekondari”  amesema Mateko Jackson

Post a Comment

0 Comments