UTAFANYAJE UKIMFUMA MPENZI WAKO ANAFANYA MAPENZI NA MTU MWINGINE??

Jamaa mmoja amezua mjadala mkali mtandaoni baada ya kuwataka mashabiki wake kusema watakavyofanya ikiwa watampata mchumba wao kitandani na mtu mwingine.

Hii ni baada ya Derrick Mbugua kumpata mpenzi wake akigawa tenda kwa mwanaume mwingine.

Kila mara Mbugua alikuwa akimshuku mpenzi wake na ndipo alipoamua kumwekea mitego ambayo ilimnasa 'live'.

Baada ya kumpigia simu usiku mzima bila ya kujibiwa, jamaa huyo aliamua kwenda kwa mpenzi wake majira ya saa tisa alfajiri.

Alipofika, alikutana na kifuli kubwa mlangoni lakini akaamua kupiga kambi mpaka kulipokucha na hapo ndipo alipomwona binti huyo akirejea kimya kimya.

Kwa sauti nyororo, Mbugua alimuuliza ni kwa nini alikuwa hayupo nyumbani kwake na ni kwa nini alikuwa akigawa tenda nje?

Katika video ambayo ameiweka mtandaoni, barobaro huyo anasikika akimuuliza jamaa anayedaiwa kula tunda lake kuhusu kujuana na mpenzi wake.

Jibu la dume huyo ni kwamba waliongea na binti huyo miaka mitatu iliyopita na walikutana ghafla na wakafufua penzi lao la zamani jibu ambalo linamshangaza sana Mbugua.

“Hujaongea na mwanamke kwa miaka mitatu na mnakutana na kushiriki ngono? Hauogopi hata kupatwa na magonjwa?” Mbugua anasikika akisema.

Mwishowe Mbugua anasema kwa kweli ni wajibu wa mpenzi wake kumlindia asali yake na hivyo hakuna haoni haja ya kumlaumu aliyeiramba.

Post a Comment

0 Comments