NA JESSCA NANGAWE
MWANADADA mjasiriamali Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole amemtaka msanii mwenzake Roma Mkatoliki kutokuachana na mkewe kama tetesi zinavyoeleza kwani kwa kufanya hivyo kutaondoa undugu wao.
Kumekua na tetesi kuwa ndoa ya Roma mkatoliki na mkewe imevunjika na kila mmoja kwa sasa kuendelea na mambo yake jambo ambalo limemuumiza sana Shilole.
Akizungumza na DIMBA, Shilole alisema, mpaka sasa msanii huyo ameshindwa kupokea simu yake bila kujua chanzo ni nini huku akimini kuwa tetesi hizo huenda ni za kweli kutokana na kumkwepa.
ìSijui kwa nini hapokeI simu yangu, nimejaribu kumpigia sana hapokei, nadhani ananiogopa na kama ni kweli amefanya hivyo, atakua amenikosea sana na nadhania undugu wetu utaishaîalisema Shilole.
0 Comments