NILIBAKWA NA RAIS WA ZAMANI

Fatou Jallow anasema kuwa alitoroka The Gambia baada ya kubakwa na sasa anaishi nchini Canada

Malkia wa urembo wa zamani nchini Gambia Fatou Jallow, amesema kuwa alibakwa na rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh 2015 wakati alipokuwa mamlakani.

Ushahidi wake ni miongoni mwa ripoti ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch ambayo inaelezea madai mengine ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na bwana Jammeh.

BBC ilijaribu kuwasiliana na bwana Jemmeh ambaye kwa sasa anaishi mafichoni Equitorila Guinea , kuhusu madai hayo.

Msemaji wa chama chake cha APPR alikana madai hayo yaliotolewa dhidi ya bwana Jammeh.

''Sisi kama chama na raia wa Gambia tumechoka na msururu wa madai ambayo yameripotiwa dhidi ya rais wa zamani'', alisema Ousman Rambo Jatta katika taarifa iliotumwa kwa BBC.

Yahya Jammeh aliitawala Gambia kwa takriban miaka 22

"Rais huyo wa zamani hana muda wa kujibu uongo na kampeni za kumuharibia jina. Ni mtu anayemuogopa mungu ambaye anaheshimu sana wanawake wa Gambia'', alisema naibu wa kiongozi wa chama hicho cha APPR.

Bi Jallow aliambia BBC alitaka kukutana na bwana Jammeh mwenye umri wa miaka 54 mahakamani ili ashtakiwe.

''Nimejaribu sana kuficha na kufutilia mbali habari hiyo na kuhakikisha kuwa haitakuwa moyoni mwangu. Kwa kweli sikuweza , hivyobasi nikaamua kuzungumza kwa sababu ni wakati wa kusema ukweli na kuhakikisha kuwa Yahya Jammeh anasikia kile alichokitenda.

Alisema kwamba pia yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya tume ya haki na maridhiano nchini Gambia TTR ambayo imebuniwa na rais Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi Disemba 2016.

Tume hiyo ya haki na maridhiano inachunguza ukiukaji wa haki za kibinaadamu wakati wa utawala wa miaka 22 wa bwana Jammeh , ikiwemo ripoti za mauaji ya kiholela , ukatili na kukamatwa na kuzuiliwa kiholela.

Alilazimishwa kutoka afisi mnamo mwezi Januari 2017 baada ya mataifa jirani kutuma vikosi vya kijeshi alipokatalia madaraka.

Alikataa kuolewa na Jammeh

Bi Jallow alisema kuwa alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipokutana na Jammeh baada ya kushinda shindano la malkia wa urembo wa 2014 katika mji mkuu wa Banjul.

Miezi kadhaa baada ya kupata taji hilo, anasema kwamba rais hyo wa zamani alijifanya kama mzazi wakati alipokutana naye akimaptia ushauri, zawadi na fedha na kuandaa maji kupelekwa katika nyumba yao ya familia.

Na katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na msaidizi wa rais huyo , anasema alimuuliza iwapo wangeoana.

Alikataa wazo hilo mbali na zawadi alizokuwa akipatiwa.

Bi Jallow anasema kuwa msaidizi huyo baadaye alisisitiza kwamba anafaa kuhudhuria sherehe ya kidini katika ikulu ya rais kama malkia wa urembo mnamo mwezi Juni 2015.

Lakini alipowasili , alipelekwa katika makao ya kibinfasi ya rais huyo.

''Ilikuwa wazi kile ambacho kingetokea'', alisema akitaja hasira ya bwana Jammeh baada ya yeye kukataa kufunga naye ndoa.

Bi Jallow anasema alipigwa kofi na kudungwa sindano katika mkono wake.

''Alifuta sehemu zake za siri katika uso wangu, akanisukuma nipige magoti na kunifanya vibaya''

Wasichana wa itifaki

Msichana huyo baadaye alisema kuwa alijifungia nyumbani kwao kwa siku tatu na kuamua kutorokea Senegal.

Alipokuwa mjini Dakra mji mkuu wa Senegal , Bi Jallow alitafuta usaidizi wa mashirika kadhaa ya haki za kibinadaamu.

Wiki chache baadaye alipatiwa ulinzi na kupelekwa nchini Canada ambapo amekuwa akiishi tangu wakati huo.

Mara kwa mara Bwana Jammeh alitembelea kijiji cha nyumbani kwake huko kanilai

Shirika la Human Rights Watch (HRW) na Trial International yanasema kuwa bwana Jammeh alikuwa na mfumo wa kunyanayasa wanawake , ambapo wanawake wengine walikua wakilipwa mshahara na serikali na kufanya kazi katika ikulu kwa jina 'wasichana wa itifaki'', ambao walikuwa wakifanya kazi za ukarani lakini umuhimu wao mkubwa ulikuwa kushiriki ngono na rais.

BBC haikuweza kubaini madai hayo, lakini afisa mmoja wa zamani nchini humo ambaye alikubali kuzungunza bila jina lake kufichuliwa alisema kuwa anajua kuhusu mambo mabaya yaliokuwa yakitendeka katika afisi ya rais: Maafisa wa itifaki walikuwa wanawake na waliajiriwa ili kuridhisha mahitaji ya rais.

Anakumbuka kumuona bi Jallow katika ikulu mara nyengine wakati wa usiku.

Post a Comment

0 Comments