NA JESSCA NANGAWE
MWANADADA Faustina Charles maarufu kama Nandy amefunguka kuwa, hawezi kutoka nyumbani kwake bila kuvaa pambo la hereni na mkufu pamoja na miwani.
Nandy ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kupitia uimbaji wake, amesisitiza kuwa amekuwa shabiki mkubwa wa mambo ya urembo ukiachilia mbali muziki wake na mara nyingi akiwa kama mwanamke anatamani sana kuonekana wa tofauti.
ìMimi ukiachilia muziki wangu napenda sana kujiweka nadhifu, napenda sana kuonekana nimependeza kila sehemu nnayokwenda, sasa huwezi kuona natoka nyumbani sijavaa hereni, mkufu ama kubeba miwani, hivi ni vitu ninavyovipa kipaumbele sana kwenye muonekano wanguîalisema Nandy.
0 Comments