MWANAFUNZI: MAMA NDIYE ALIYENILAZIMISHA KWENDA KULALA NA ASKARI

Mwanafunzi anayedaiwa kupewa ujauzito na askari wa polisi mkoani Mbeya aeleza jinsi mama mkubwa alivyochonga mchongo wa kuwakutanisha na kumlazimisha kutoa penzi kwa askari huyo akiwa lindoni mkoani Mbeya.

Mwanafunzi huyo ambaye amefukuzwa shule na walimu alikuwa anasoma kidato cha kwanza ana umri wa miaka 14 jina lake tumelihifadhi alipatiwa mimba Desemba mwaka jana na askari huyo.

Alisema askari huyo alimpigia simu mama yake mkubwa Ashura Abdalah “Sijajua waliongea nini ila mama mkubwa alinifuata na kuniambia Daniel anakuita siku ya kwanza nilikataa siku ya pili tukaenda,”

Alisema siku ya tatu ambayo ilikuwa ni Desemba “Mama mkubwa alisimama pale chini mlangoni mimi nikapanda kule juu Daniel akanivua nguo na kuingiza uume wake katika uchi wangu baada ya kumaliza alinipatia Sh. 5,000,” alisema.

Aliongezea kuwa:”Nilivyotoka nje akabaki na mama mkubwa ndani baada ya muda mama mkubwa alitoka na kuniambia tuondoke nyumbani. Siku ya kwanza nilivyokataa alinifokea akaniambia ole wako umuambie mtu nikaa kimya siku ya pili akanimbia twende nikaa pale kwenye ngazi nikakataa kufanya hicho kitendo,”

Mama wa mtoto huyo Aisha Mohamed, alisema alipatiwa taarifa na mjomba wake kuwa mwanae ana mimba ya miezi mitano jambo ambalo lilimshangaza.

“Nikauliza ina maana mwanangu alivyokuwa anasubiria majibu alikuwa ni mjamzito akanijibu hafahamu ila ameanguka shuleni na alivyokwenda kupimwa akakutwa na ujauzito kwa hiyo wakuwalaumu ni bibi yake na mama yake mkubwa ambao Wanakaa naye,” alisema

Alisema baada ya kupatiwa taarifa hizo alikwenda kumuona mtoto wake ilivyopita siku mbili askari huyo ametoroka na mpaka sasa hajajua kinachoendelea.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Sebastiani Mbuta, alisema tuhuma za askari huyo wamezipata na hatua za kinidhamu zitaendelea.

Alisema askari huyo alitakiwa kuingia kazini lakini hajaonekana baada ya kudaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi.

Post a Comment

0 Comments