MAMBO 9 YANAYOWAVUTIA WANAUME KWENYE MAPENZI

Wanawake wengi hudhani kwamba, wanaume huwa hawachunguzi vijimambo vidogo dogo kwamba wanachojali ni muonekano tu, kama mzuri mzuri tu.

Ukweli ni kwamba dhana hiyo si ya ukweli. Ingawa wanaume huangalia vitu vinavyoonekana kwa mara ya kwanza, huwa wanajali kuhusu kila kitu.

Wanajali kuhusu nini unaongea, jinsi gani unaongea, muonekano wako, maono yako, mtindo wako wa maisha, mavazi na vingine.

Wanaweza wasiseme lolote, lakini amini kwamba wanavichunguza vitu hivyo. Je unahitaji kujua vitu hivyo? Ngoja tuviongelee vitu 9 ambavyo wanaume huvitazama au huvichunguza ndani ya mwanamke hata kama unahisi hawajali kuhusu hivyo:

Staili yako ya Mavazi

Si wanaume wote watajua fasheni gani ipo juu kwa sasa, kwamba sasa hivi kuvaa hivi au vile ndo fasheni, lakini amini usiamini kama unajua fasheni atakuona tuu na atakusifia kama umependeza bila kujali kwamba umevaa kitu cha ghali au gharama nafuu.

Kucha

Wanawake wengi hutengeneza kucha kujifurahisha wenyewe  au kuwaonyesha mashosti zao, kwamba wanaume hawana mda na kucha hizo. Ukweli ni kwamba wanaume pia huwa wanaziangalia, wanazichunguza na wanapenda msichana awe na kucha nzuri za kuvutia.

Sasa hapa si lazima mwanamke uweke makucha kama kitu gani sijui, ziwe tu nzuri, simple, za kuvutia, safi na zilizofanyiwa huduma. Hii itamjulisha mwanaumwe kwamba wewe ni msafi na unajali muonekabo wako.

Jinsi ulivyo

Hapa nazungumzia tabia kiujumla, tabia yako ndio itakayokufanya mwanaume abaki au aondoke na ukweli ni kwamba, wanaume hawapendi mwanamke mjeuri asiye na busara wala kauli nzuri. Watu wote kwa ujumla bila kujali jinsia wanapenda mtu ambaye kua nae ni raha na si karaha.

Manukato

Unaweza ukashangaa kuhusu hili, lakini wanaume wanapenda manukato mazuri. Watu huwa wanatabia ya kueka kumbukumbu ya manukato, na ikitokea ukayasikia sehemu nyingine basi unamkumbuka mtu au hata sehemu mliyokuwa wote akiwa ananukia.

Mwanaume atakumbuka manukato yako mwilini au hata jinsi nywele zako zinavyonukia vizuri kutokana na mafuta mazuri au hata marashi ya sabuni uliyooshea nywele. Sasa vipi kama una wigi kichwani miezi miwili na huna mpango wa kulitoa na unaenda kukutana na mpenzi? Manukato ni muhimu wadada/wamama.

Maisha ya kijamii

Unaweza kujikuta unasahau maisha mengine ukiwa na mwenzi, lakini wanaume hupenda wanawake ambao wanaishi maisha yao nnje ya mahusiano. Inawaonyesha kwamba wewe ni mtu wa kujichanganya, na watu wanapenda kuwa na wewe. Si mbaya mara moja moja kutoka na marafiki zako.

Furaha

Mwanaume siku zote atapenda uwe mtu wa furaha, sio kununa nuna. Haimaanishi kwamba uwe unatabasamu mda wote, lakini walau uwe mtu mwenye muonekano wa furaha na sio mda wote uonekane kama una hasira au msongo wa mawazo.

Kujikubali

Kila mtu anajua hakuna kitu kizuri kama kujiamini na kujikubali. Wanawake hupenda wanaume wanaojiamini na kujikubali, basi na kwa wanaume ni hivyo hivyo. Si vizuri kuwa na mtu ambaye kila wakati anahofu na hajikubali.

Mchekeshaji

Wanaume hupenda mtu ambaye anaweza kumchekesha walau kidogo, ile unakuta mtu kaongea kitu unacheka si suala la kua kama kina joti. Si lazima kila siku yeye ndo achekeshe, siku moja moja na wewe uwe unamchekesha mwenzio na mtaonekana kuwa wapenzi wenye furaha siku zote machoni mwa watu.

Moyo Mkunjufu

Mara nyingi tunaaminishwa kuwa wanaume wana shida na kitu kimoja tu, nadhani ushaelewa hapo. Lakini ukweli ni kwamba hata wao wanahitaji sana kupendwa, si lazima hicho kitendo. Na kwa sababu mara nyingi wao ndo huanza kusema kuhusu hisia zao, itakua ni vyema kama utakua mkweli pia kuhusu hisia zako na madhumuni yako.

Post a Comment

0 Comments